Mkuu
chiembe , TBC ni TV yetu ya Taifa, unapolalamikia tatizo lolote la TBC, kwanza tanguliza uzalendo wako kwa taifa lako, kisha unalitaja tatizo uliloona kwa TBC.
Kwenye bandiko hili, umelalamika tuu kama unanenemeka, bila kusema mtangazaji huyo unayemlalamikia amefanya makosa gani ya kiutangazaji hadi wewe kulalamika.
Tuanzie hapa
1. Taja jina la mtangazaji husika
2. UWT ni Jumaiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi, hivyo ni chama cha Wanawake wa CCM, hapo hakuna tatizo lolote,!.
3. Kama kuna tatizo jingine litaje
watangazaji hawapangiwa majukumu ya utangazaji kwa seniority bali kwa ability, capacity, capability na talent.
Ability ni uwezo wa utangazaji, kila mtangazaji wa TBC ana uwezo wa kutangaza chochote ndio maana ameajiriwa.
Capacity ni uwezo binafsi wa mtangazaji kuitanga tukio fulani unatofautiana mtu na mtu, kuna wengine wana uwezo mkubwa wengine mdogo.
Capability ni kujengewa uwezo wa kutangaza tukio lolote hivyo watangazaji wote wa TBC wakifika TBC wanapikwa upya. Kukitokea tukio la Msikitini anapekekwa mtangazaji Muislam, la kanisani Mkristu etc
Talents huu ni uwezo binafsi wa kipaji cha mtangazaji kutangaza jambo fulani ndio maana sio kila mtangazaji ni mtangazaji wa habari, mpira, muziki, au kuwa anchor. Watangazaji tofauti wana vipaji tofauti hivyo wanapangiwa kutokana na vipaji vyao.
Seniority ina mater kwenye kukabidhiwa majukumu na madaraka
Hapa sasa ndipo palihitaji uzalendo
Haiwezekani mazuri yote ya TBC usiyaone na kutukana hovyo kabisa!.
Haya ni baadhi
- Live News Interactive!-TBC-1 Yastahili Pongezi!. ''Hongera TBC-1" Keep it Up!
- Elections 2010 - Uchaguzi 2010: TBC1 are doing good job!
- TBC Yafanya Kweli!, Yashusha OB Van ya Kufa Mtu!, Ina Kamera 12!. Itarusha HDV Signal Kama DSTV.
- Watangazaji Wetu na elimu zao
- Dr. Ayub Rioba atoa Mwelekeo wa TBC kwa Mwaka 2018. Kufikisha viwango vya juu kiwango cha BBC
- Kampeni UKAWA: Mnyonge Mnyongeni!, TBC, Inastahili Pongezi!, Jana Imefanya Kazi Nzuri Iliyotukuka!
- Television ya Taifa,TBC, Imetisha!. Yarusha Live Mbili Kwa Wakati Mmoja! Live ya Dodoma on TBC1 At the Same Time Live ya Arusha TBC2- Safari Channel
- Safari ya Mwisho ya Mwanahabari Nguli wa Siasa, Marin Hassan Marine, Alianzisha Jambo TZ na Ameacha Alama ya TBC Aridhio
- Tribute to Halima Mchuka: Alikuwa Mtu wa Watu!
- Tribute to Halima Mchuka: Miaka 10 Baada ya Kifo Chake, Her Legacy Still Lives On!, Bado Ndiye "The One and Only" Mtangazaji wa Kike wa Mpira Bongo!.
- Mtangazaji wa TBC, Aboubakar Mwanamboka, afariki Dunia!
- TANZIA - Mtangazaji Maarufu wa RTD Abissay Stephen amefariki dunia asubuhi hii
- Tribute To Uncle J. Nyaisanga: Jee Unamkumbuka kwa Lipi?!. Kuagwa Leo Leaders Club!
- Tribute to David Wakati, Kikwete, Mengi, Nchimbi na wengine, Wamzungumzia David Wakati (TBC Live)
Sasa hayo yote huyaoni wewe unasema TBC hovyo kabisa!. Its not fair!.
P.