ITV na Radio one, kama mzee Mengi hatabadiri management zake, kwangu mimi naona anajiandalia kifo cha vituo hivyo.
nasema haya kwasababu, viongozi wake hawana ubunifu wakisasa, hawana mbinu za kukabiliana na changamoto za maisha ya kisasa.
ITV inaendeshwa vilevile kama miaka kumi iliyopitwa, kwa kuangalia mtiririko wa vipindi, uwasilishaji wake na hata haiba ya watangazaji wake.
Radio One, ndo kabisa, hata akifufuka leo mtu aliekufa mwaka 2000, ataweza kukupa ratiba nzima ya vipindi bila taabu.
hii ni ishara ya uongozi uliofulia, uongozi unaokopi na kupaste yaleyale.
ITV/Radio One KUGOMEA MECHI ZA SIMBA, hiki nacho ni kielelezo cha uongozi wenye fikra mgando, wanatumia majungu na fitina na hata mapenzi yao binafsi kuihukumu na kuinyonga SIMBA.
Kama hawakuwa na maslahi binafsi ni kwanini iwaume Simba kugomea Mechi zao kuonyeshwa ?
mbona imewauma sana ? mbona Star TV wanaendelea kama kawa na matangazo yao kuihusu Simba ?
Deo Rweyunga na Issack Gamba plus KitenGE Maulid, mmeumbuka ama Mmmeumbuliwa na Kaduguda, Fitina zenu hazitashinda.