Padre
Charles Kitima ni katibu wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania
(TEC) ambaye alipata daraja takatifu ya upadre takribani miaka 27 iliyopita ambapo mwaka 2022 aliadhimisha Jubilei ya miaka 25 ya Upadre katika Parokia ya Kristu Mfalme Siuyu Jimbo Katoliki Singida mahali alipozaliwa.
Padre Kitima amekuwa ni moja kati ya viongozi wa kidini ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa
elimu ya urai kwa wananchi sambamba na
kukemea na kukosoa maovu, uvunjwaji wa haki za binadamu na taratibu za kidemokrasia. Vilevile amekuwa ni mkosoaji wa serikali katika utendaji wake ili kuhamasisha uwajibikaji na utawala bora nchini.
Baadhi ya watu wasio na nia njema mara kadhaa wamekuwa wakitoa taarifa zinazopotosha kumhusu padri huyo, tazama
hapa na
hapa.
Hivi karibuni kumeibuka machapisho yanayosambaa mitandaoni yakidaiwa kuchapishwa na vyombo vya habari vya TBC (Tanzania Broadcasting Corporation) na ITV (Independent Television) yakiwa na kichwa cha habari kinachosema ‘Mazito ya Neema na Kitima yafichuka’
Je ni upi uhalisia wa machapisho hayo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa taarifa hiyo haijachapishwa na vyombo vya habari vya
ITV na
TBC na haina ukweli wowote kwani haijataja chanzo cha kuaminika dhidi ya madai yanayohusishwa na taarifa hiyo.
Aidha JamiiCheck imebaini mapungufu kadhaa katika machapisho hayo ambapo,
Chapisho lililotumia alama na nembo ya TBC limeongezewa alama ya rangi nyeupe katikati ya sehemu inayotenganisha eneo linalowekwa kichwa cha habari na upande uliowekwa neno ‘updates’ kitu ambacho ni tofauti na machapisho halisi ya TBC ambayo sehemu hiyo huachwa wazi.
Vilevile
Chapisho lililotumia nembo na alama za
ITV limetumia mwandiko tofauti na ule unaotumiwa na chombo hicho cha habari katika machapisho yake rasmi katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, sanjari na hilo pia sehemu inayobeba kichwa cha habari haionyeshi picha iliyowekwa nyuma yake tofauti na
machapisho rasmi.