TBC1 HD Itumike kurusha matangazo ya mpira

TBC1 HD Itumike kurusha matangazo ya mpira

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2014
Posts
3,292
Reaction score
7,867
Ndugu wanabodi wakati kombe la Dunia likielekea ukingoni Kuna vitu vimenivutia. Baadhi ya vitu hivyo ni watangazaji na wachambuzi. Hapa unakutana na NAZARETH UPETE Kama mtangazaji na huku RAMADHAN MBWADUKE Kama mchambuzi.

Hawa jamaa ni hatari na nusu hasa mchambuzi anakuchambulia wachezaji wote background zao, mfumo wa kocha, Nini wafanye Ili kushinda bila kuegemea upande Wala kuingiza ushabiki mpaka unapenda dk ziongezwe.

Masikitiko yangu ni kuwa huyu dingi RAMADHAN MBWADUKE na mwenzake NAZARETH UPETE hatutawasikia Tena baada ya hili mbungi. Kama ingewapendeza TBC waturushiage hata mechi mbili Kwa wiki sio mbaya Ili tunufaike nao.


Leo watakuwa liveView attachment 2434450
 
Mkuu wasikilize jamaa hawa Gharib Mzinga na Ramadhan Ngoda na katika uchambuzi kuna jamaa anaitwa George Ambangile... kwa upande wangu wapo vizuri sana sana
 
Mkuu wasikilize jamaa hawa Gharib Mzinga na Ramadhan Ngoda na katika uchambuzi kuna jamaa anaitwa George Ambangile... kwa upande wangu wapo vizuri sana sana
Huwa nawasikiliza Sana tu mkuu ila RAMADHAN MBWADUKE kawapiga gepu Sana. Hata kwenye page ya Salama Ngale ya Facebook kampost huyo mwamba.
 
FTA Ila wangeweza kufanya maboresho madogo tu ingekuwa poa Sana.
Kurusha video HD unalipia, sasa TBC wanaweza kulipia mechi zote.? Tangu nimeanza kuangalia WC kupitia TBC ni mara moja tuu wameonyesha WC kwa HD
 
Uyo Nazareth upete [emoji28][emoji119][emoji119] ni noma nimemfatilia baadhi ya mechi na nimemuelewa

Anasherehesha vzr sna
 
Back
Top Bottom