Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
Leo Maktaba imetembelewa na TBC1 kufanya kipindi kuadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani.
Mtangazaji wa TBC1 Hilda Sengoli alitaka tuzungumze mchango wa Kiswahili katika kuwaunganisha Watanganyika kama watu wa taifa moja kupigania uhuru wa Tanganyika.
Nilimfahamisha kuwa Kiswahili kinakwenda na Ushairi na Mwalimu Nyerere Rais wa TANU na kiongozi wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika alikuwa mshairi wa sifa na TANU haikuwa na upungufu wa washairi.
Niliwataja baadhi ya washairi ndani ya TANU yenyewe nikiianza na Mwalimu kama mshairi, Kaluta Amri Abeid, Saadan Abdu Kandoro, jina lake la ushairi, ''Ustaharaki'' Shaaban Gonga hawa kama nilivyosema walikuwa ndani ya TANU.
Kulikuwa na washairi bingwa nje ya TANU lakini wazalendo na walidhihirisha uzalendo wao katika mashairi waliyotunga ya kuhamasisha umma kusimama kuipigania nchi yao hadi iwe huru mshairi kama Mohamed Selemani.
Mohamed Selemani jina lake la ushairi lilikuwa ''Mtu Chake.''
Mtu chake alikuwa akitunga mashairi ya kuhamasisha uhuru na kuwapiga vijembe Waingereza kiasi alikamatwa lakini serikali ilkashindwa kumsimamisha kizimbani mahakamani pengine kwa kohofia vijembe zaidi katika tungo za washairi katika kumtetea mwenzao.
Kisa cha Mshairi ''Mtu Chake'' kipo katika kitabu cha Abdul Sykes.
Kwa kuwa imesadifu leo kuwa ndiyo ilipoasisiwa TANU nilieleza jinsi TANU ilivyokipigania Kiswahili kuwa lugha ya taifa baada ya Tanganyika kupata uhuru wa wake mwaka wa 1961.
Hakika Kiswahili kilikuwa lugha ya uhuru wa watu wa Tanganyika.
View: https://youtu.be/o-bfKCmDV3A