TBL na Serengeti Bia



Sasa SBL mtanikamata vizuri make huko kwenye spirit nako nipo na karibu mna brand zote nipendazo.

Mkuu Kidumempiganaji, vipi kuhusu Mohans? Si ndo muuzaji wa vitu hivi au hana exclusive right?
 

Ewaaaa Mkuu. Ubarikiwe. Achana na kojozi la serengeti. Full kuchamba koo.
 


Acheni kunywa mabeer yanaharibu afya kwa kuleta vitambi, kwanini msiwe kama mimi




Ama

 
Yatawashinda TBL tu mimi naamini ushindani mzuri sio kuzibiana ila ni kuongeza ubora full stop, haya mengine ni kuweweseka tu
 
Kweli nimeamini JF watu wa maji mpo,maana mko full force!
 
Acheni kunywa mabeer yanaharibu afya kwa kuleta vitambi, kwanini msiwe kama mimi




Ama


Kwa kiingereza changu cha shule ya kata, nakumbuka hivi vimaneno...........The pudding of the food lies in eating and the beauty of the thing is in the eyes of the beholder!
 

Inawezekana, si unajua tena yale maeneo yanaitwa Nyaishozi. Mitaa ya kwetu ile swahiba.
 
na jana nilikuwa hongera baa sinza hamna, tukaenda topland bar magomeni hola, tukahamia highway bar nako patupu kasheshe hupati Chui kafichika! ila nafikiri akitoka huyu chui atauma sana watu. Chuiiiiiii uko wapi

TBL wamefulia na fire extinguishers zao, CHUI anatisha. Uzuri wa chui, kuna take away, hata wakizibania uswazi, supermarket zipo kibao hadi kwa Mohans zinapatikana! Wakawaonge basi na shoprite ama samaki samaki!
 
kuna kipindi flani serengeti ilikuwa juu tbl wakaona style ya kuiondoa sokoni ni kuzinunua bia zaserengeti zote kwenye bar mapemaaaaaa asubuhi,kwahiyo ukienda mida ya mchana kupata kilaji unaambiwa serengeti zimeisha,na unaamua kuagiza bia nyingine ambayo itakuwa ya tbl,walifanya hivyo wakiamini kwa muda fulani wa kufanya hivyo wanywaji watazoea kunywa bia yao na kusahau serengeti,lakini iliposhtukiwa hiyo deal,serengeti wakaongeza uzalishaji na usambazaji wa kilaji yao,basi ikawa mkusanyaji wa tbl akipita tu kukusanya,baada ya muda msambazaji wa serengeti anapitisha tena,ikifika jioni tbl na serengeti wote wapo mezani kama kawa, tbl wakaamua kuacha kamchezo.sasa naona wameamua kuja na style nyingine,na hivi wametuharibia kilaji yetu ya ndovu basi watafulia sanaaaaaa
 

sanawari mpaka kwa morombo???????
pale city garden sanawari chui wapo wa kutosha mkuu usihofu
 


Nasikia bia ya ndovu ni uzuri wa mkakasi tu, wameongeza alch kutoka 4.2 to 4.8
 
TBL tabia yao katika competition siyo nzuri hata kidogo. Tukumbuke kuwa waliwahi kuzuia agents wao wasiuze heineken, jamaa wa heineken wakaenda mahakamani TBL wakashindwa kesi.

EABL wamekuja na mpango wa kununua shares serengeti ili waweze kupitisha bia zao pale,TBL wameenda mahakamani. Kama bia ni nzuri waache tu,wateja watachagua. Jamaa wana competition y a kitoto sana.

Jamani wanywa serengeti endeleeni,kwanza TBL walikuwa wanadhamini ligi ya bongo,lakini walivyokuja hawa makaburu wakajitoa. Faida yote wanayopata, hakuna wanachotufanyia watanzania kama namna ya kushare faida. Serengeti tumejionea misaada wanayotoa kwa timu ya taifa. Kama kodi wote wanalipa,ilitakiwa kuwe na kitu cha ziada kama udhamini wa michezo.
 
Kama kweli TBL wanafanya hivyo basi si sahihi. Ila ninachojua ni kwamba sioni tofauti ya TBL na EABL, wote ni wakuja na faida itaenda ama Kenya au Bondeni. Wanaoshabikia EABL kuingia Serengeti wanaupeo mdogo hasa katika hii ushindani wa kuhodhi soko la East Africa. Nimebaki mashabiki tu wa uchumi huku wenzetu Kenya wanakimbia. Leo hii Tanzania kuna Benki ya Kenya, East African Cable ni Wakenya, Wananunua Ardhi kwa bei yeyote ile, moheteli yote ya kitalii ni Wakenya n.k. Tanzania hutufikirii na hata hatuna ubavu wa kuweka kitu Nairobi.

Tuamke jamani - achana na kushabikia ujinga.
 
na jana wameenda lillies pub msasani , nguruko mbezi wamengoa matangazo yanayowaka wakamuoffer meneja 30elfu akakataa wakangoa meneja akalichukua akaliweka yaani hawa watu wamedhamiria kweli inabidi serikali
 
TBL waling'oa mitambo ya Kibo kuipeleka Mbeya mpaka leo zinaoza kwa kushindwa kujenga kutokana na kesi ya kiwanja kuwa mahakamani.
Sasa SBL wanajenga kiwanda Moshi na hii inawaudhi sana TBL hawana raha na wanajuta waliifunga Kibo.
Pia bia ya TBL wameumia zaidi baada ya EABL kuamua Tusker itengenezwe SBL.
Sasa huyu marketing director wao inabidi kwanza afukuzwe kazi na kampuni kushitakiwa kwa CFC.
 
na jana wameenda lillies pub msasani , nguruko mbezi wamengoa matangazo yanayowaka wakamuoffer meneja 30elfu akakataa wakangoa meneja akalichukua akaliweka yaani hawa watu wamedhamiria kweli inabidi serikali

Hii sasa ndo wanaonesha kabisa wamefulia-kimarketing! Yaani wanang'oa mabango wanafikiri tutaihama Serengeti? Mi naona marketing team wameuza timu! hapa lazima refa kaongwa!
 
Hii sasa ndo wanaonesha kabisa wamefulia-kimarketing! Yaani wanang'oa mabango wanafikiri tutaihama Serengeti? Mi naona marketing team wameuza timu! hapa lazima refa kaongwa!


Serengeti! serengeti!
Serengeti! serengeti!
Serengeti! serengeti
!
 
Serengeti! serengeti!
Serengeti! serengeti!
Serengeti! serengeti!

Kaka nina kaugonjwa kakusahau kidogo! Huu ubeti ni ule wa AKUDO ama tangazo jipya la chui. Ila tuache utani Chui anafunika mkUU!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…