TBS ina Maabara 9 zinazotumika kuchunguza bidhaa kisasa

TBS ina Maabara 9 zinazotumika kuchunguza bidhaa kisasa

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
TBS INA JUMLA YA MAABARA 9 AMBAZO ZINATUMIKA KUCHUNGUZI BIDHAA KISASA

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lina jumla ya maabara tisa ambazo zinatumika katika uchunguzi wa bidhaa mbalimbali ambazo ni bora na kuna vifaa vya kisasa vya uchunguzi pamoja na wataalamu waliobobea katika uchunguzi.

Ameyasema hayo leo Meneja wa Upimaji (TBS), Bw.Joseph Makene wakati akitoa taarifa juu ya ufanyaji kazi wa maabara hizo zilizopo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Bw.Makene amesema TBS ina maabara za kupima nguo na ngozi, maabara hizo zinatumika katika uchunguzi wa bidhaa zote zinazohusu nguo na ngozi pia kuna maabara za kupima vifaa vya kikemikali ambayo hutumika kupima vipodozi pamoja na bidhaa zote za petroli.

Amesema kuna maabara ya Microbiolojia "Maabara hii inafanya uchunguzi wa uwepo wa vimelea vya magonjwa katika bidhaa zote ambazo zinapatikana nchini". Amesema Bw.Makene.

Aidha Bw.Makene amesema TBS ina maabara tatu za uhandisi ambapo kuna maabara ya uhandisi umeme ambayo inafanya uchunguzi wa vifaa vyote ambavyo vinahusiana na umeme kama vile Tv,simu, kompyuta na vingine vingi.

Amesema kuna maabara ya uhandisi mitambo ambayo inafanya uchunguzi wa bidhaa zote zinazohusu mitambo.

Vilevile amesema kuna maabara ya Ujenzi "Maabara hii inapima bidhaa zote za ujenzi kama mabomba yanayotumika katika kupitisha maji majumbani kwetu na kwenye miradi mbalimbali". Amesema Bw.Makene.

Hata hivyo kuna maabara zingine ambazo ni maabara ya kupima vifungashio na maabara ya ugezi ambayo inafanya ugezi wa vipimo vyote ambavyo vinatumika katika uzalishaji viwandani pamoja na kwenye hospitali.

Screenshot_20210826-071759.png
Screenshot_20210826-071835.png

Screenshot_20210826-071845.png

Screenshot_20210826-071906.png

IMG_20210826_072553_011.jpg
 
plus maabara moja ya rushwa kuruhusu bidhaa feki kuzagaa mitaani
 
TBS ndio chanzo cha vitu vya ajabu ajabu kutoka China
 
Back
Top Bottom