TBS: Kuanzia 01 Machi 2021, utaratibu wa kukagua magari kutoka nje ya nchi, utafanyikia hapa nchini

TBS: Kuanzia 01 Machi 2021, utaratibu wa kukagua magari kutoka nje ya nchi, utafanyikia hapa nchini

Ze Heby

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Posts
5,636
Reaction score
6,178
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linawataarifu waagizaji na wauzaji wa magari kutoka nje ya nchi kuwa kuanzia tarehe 01 mwezi Machi, 2021, utaratibu wa kukagua magarikutoka nje ya nchi utafanyika baada ya kuwasili hapa nchini (Destination Inspection). Hivyo,magari yote yatakayosafirishwa kuanzia tarehe tajwa hapo juu yatakaguliwa katika bandari yaDar-es-Salaam.

Kwa sasa TBS inakagua magari kutoka nje ya nchi kupitia mawakala watatu(3) kutoka Japan na mmoja(1) kutoka Dubai ambao mikataba yao itakoma hivi karibuni.

Hivyo vyeti vya ukaguzi vitakavyotolewa na mawakala tajwa kwa magari yatakayosafirishwa kuanzia tarehe 01 mwezi Machi, 2021 havitatambulika na TBS.

Aidha,magari yatakayopimwa bandarini na kutokidhi matakwa ya kiwango yatahitaji kufanyiwa matengenezo nje ya bandari na kisha kuletwa na kupimwa tena kwenye yadi ya UDA mkabala na Bandari ya Dar es salaam.

Shirika litaendelea kuhakikisha kuwa magari yote yaliyotumika nakuingizwa nchini yanakidhi matakwa ya kiwango cha magari yaliyotumika.

Kwa taarifa zaidi kuhusu utaratibu huu mpyausisite kuwasiliana na:-

Mkurugenzi Mkuu,

Shirika la Viwango Tanzania (TBS),

SLP 9524,

Dar es Salaam.

2671485_IMG-20210120-WA0036.jpg
 
TBS wamesajiliwa rasmi kuwa tawi la TRA, kama walivyo Trafic/Mahakama/Mgambo Wa Halmashauri na DPP. Hongereni kwa kuzindua njia mpya ya kukusanya mapato.

Siku wakikosa mapato, hata kama gari umeagiza ni jipya, utaambiwa sio rafiki kwa matumizi ya binaadamu. Unapigwa fine.
 
Wanakagua nini kwa kuanzia?

Mengi yameshakuwa nje ya specs tayari ndo maana yanauzwa kwetu maskini.

Au wanapanua goli ili kupiga pesa.
 
Hakuna watu siwaamini kama Tbs kwani kuna vitu bingo fake nchini na tbs wapo wapo tuu.Mfanobati za msauzi pale buguruni ni fake na zinauzwa ukinunua baada ya miezi kadhaa zimepauka zote.kiufupi hapo hamna kitu now tutakuwa taifa la kuingiziwa bidhaa dhaifu.
 
Hapa naona vitu vifuatavyo;

1. Hata kama gari itakuja nzima, utaambiwa ni mbovu. Linatakiwa likatengenezwe. Kuna vifaa vitachomolewa halafu utavikuta kwenye garage zao uuziwe mara ya pili.

2. Watalazimisha wapeleke garage zao. Bei zitakuja za ajabu. Usishangae ukaambiwa ulipe 500K kwa kitu ambacho ungetengeneza kwa 200K.

3. Ukaguzi utachelewa vibaya sana. Gari limefika tar 1 ila litasubiri ukaguzi wa ndani kwa mwezi mzima. Ndo mtambiwa, mkaguzi amesafiri kwenda dodoma. Subirini mpaka week ijayo. Au umeme hakuna, nendeni mrudi baadae.
 
Back
Top Bottom