TBS mmelala usingizi

NSHOMA FRANCOUS

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2012
Posts
698
Reaction score
325
JPM tutumbulie hawa watu..wanyonge tunapa tabu sana,kuna vifaa feki vinaingia ,kwa mfano hivi sijui wanaviita burners vya majiko ya gesi madogo ,ni feki sana!wameleta feki vinaharibika mapema na sokoni vimemwagwa vingiii ili tununue in routine basis..huu ni utapeli wa wazi kabsa.TBS mmelala usingizi tena wa pono.
 
POLE SANA MKUU,HAKUNA TAASISI IMEJAA VILAZA KAMA TBS.KUNA BIDHAA NYINGI MNOOOOOO FEKI HASA KUTOKA CHINA NA ZIKO SOKONI
 
Wapo busy na Lotion na vipodozi tu. Tanzania kuna vitu feki kila mahala mpaka mademu fake ukikutana nae harusi usiku ukimuona asubuhi sio yeye sababu ya makeup.
 
Halafu wana jengo kubwa jipya zuri, humo ndani wanafanya nini badala ya kudhibiti bidhaa fake
 
Wewe mwenyewe umetumia jina feki huku
 
WEKA picha tuone Mkuu tuone yalivyo tusiingie mkenge
 
bila kusahau memory card na flash feki unauziwa flashi ukiweka nyimbo 30 ujue zita pray mbili tu
 
Ukiwauliza wanakwambia hawana utaalam na hivyo vitu hivyo hawana standards za kulinganishia ubora
 
Hii nchi imejaa takataka nyingi sana kutoka china. Pamoja na vifaa vingi hasa vya kielectronic vinavyouzwa soko la ulaya kutoka china lakini hawathubutu kupeleka vitu ambavyo ni sub-standard. Kwa hiyo mchina anatumia udhaifu wa regulatory bodies kwenye nchi za kiafrika kujaza takataka kwenye masoko ya afrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…