Mambo yamekuwa magumu sana
Bila kutoa kitu kidogo au connections basi salama yako itakuwa gari itakaguliwa hata miezi miwili na utaipata upande mwengine gari itakaa muda mrefu au mfupi na utaambiwa ni bovu ulipie gharama wanayotala wakurekebishie.
Na kadri mchezo utavyonoga basi hata gari likiwa zima halina tatizo utaambiwa tu ni bovu na utatoa hela ya matengenezo .
Mbaya zaidi mtu anaweza kuchomia spea ya gari yako ambayo haina tatizo lolote akaiweka kwenye gari yake au ndugu yake akakuwekea spea kuu kuu na bado ukalazimika kutengeneza gari kwa gharama kubwa
Usalama wa spea za magari yetu na spea utakuwa mdogo sana, hebu vuta picha mkaguzi au fundi anatesti gari yako akiigongesha je?, na huko gereji itapokuwa inalala kuna baadhi ya mafundi wezi hawa ulinzi wa spea zetu upoje?
Na usiombee uwe na adui hapo tbs, huchomoki, utapigwa hela ya matengenezo hadi akili ikae sawa.
Kwa hili linalotaka kufanyika kiukweli mnakatisha watu tamaa kuagiza magari kutoka nje, Yani sipendi gari nayoagiza kufunguliwa kwajili ya ukaguzi na wabongo maana tunajuana vizuri, Kwa hali hii ukiagiza gari tenga hela ya matengenezo kabisa lasivyo utaumizwa sana na gharama za kutunza gari gereji na hatimae kulitelekeza.
Tbs kwa hili mmekurupuka.