Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Miaka ya hivi karibuni kumezuka viwanda vingi sana mitaani vinavyosaga unga wa mahindi na muhogo, ubora wa unga huo u atia mashaka kwani viwanda husika haviko kwenye usafi unaoridhisha.
Kiwanda ambacho hakiko kwenye usafi hata ubora wa unga wake utatia shaka, ni wazi viwanda hivyo vina mashine ya kukoboa na kusaga, havina mashine ya kusafisha nafaka husika hivyo kunauwezekano mkubwa kusagwa na takataka nyingine.
Nafaka zinazopatikana miaka hii huwa na uwezekano wa kuathirika na sumu kuvu na sumu zitokanazo na madawa ya kuhifadhia nafaka pamoja na ya kuua wadudu mashambani, haya yote ni hatari kwa afya zetu.
Ni jambo lililo wazi nchini kwetu hakuna utamaduni wa kichukua sampuli madukani na kwenda kuzipima maabara, TBS na TFDA nendeni madukani mchukue sampuli mkazipime naamini matokeo yatalishitua taifa kutokana na utitiri wa viwanda vya vichochoroni.