Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
- Thread starter
- #21
Hii nayo itapita bila hatua zozote kuchukuliwa labda aseme Waziri Mkuu au Rais.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndiyo hivyo mkuuNi ngumu sana kwa TBS wapime ubora wa kondomu, soksi, magari, khanga, matofali, mita za maji na umeme hata bendera ya taifa na vyote tunavyotumia nchini waweze kupima ubora wa unga! Ni ukweli usiopingika kuwa hawapimi unga uliozagaa mitaani, pia biashara hiyo imeachwa holela mpaka vichochoroni na haijawahi kuwa na muongozo wowote ule, tunakufa taratibu na hakuna anayejali.
TBS na TFDA kazi kubwa wanayo fanya ni kwenda kuuza sura kwenye maonesho ya sabasaba na mengineyo. Hata ukiwaona kwenye tv ni pale wanapo shika vipodozi na viwatilifu kwenye viduka. Bidhaa nyingi ziingizwazo na kuzalishwa nchini ni mbovu na hata washikwao huishia kuelewana.Miaka ya hivi karibuni kumezuka viwanda vingi sana mitaani vinavyosaga unga wa mahindi na muhogo, ubora wa unga huo u atia mashaka kwani viwanda husika haviko kwenye usafi unaoridhisha.
Kiwanda ambacho hakiko kwenye usafi hata ubora wa unga wake utatia shaka, ni wazi viwanda hivyo vina mashine ya kukoboa na kusaga, havina mashine ya kusafisha nafaka husika hivyo kunauwezekano mkubwa kusagwa na takataka nyingine.
Nafaka zinazopatikana miaka hii huwa na uwezekano wa kuathirika na sumu kuvu na sumu zitokanazo na madawa ya kuhifadhia nafaka pamoja na ya kuua wadudu mashambani, haya yote ni hatari kwa afya zetu.
Ni jambo lililo wazi nchini kwetu hakuna utamaduni wa kichukua sampuli madukani na kwenda kuzipima maabara, TBS na TFDA nendeni madukani mchukue sampuli mkazipime naamini matokeo yatalishitua taifa kutokana na utitiri wa viwanda vya vichochoroni.
Hili la sumu kwenye nafaka hivi sasa ni tatizo kubwa sana huku wanaotakiwa kudbibiti wanalipuuzia kama vile hakuna tatizo!Unakuta umepiga mahindi dawa ili uhifadhi kwa matumizi ya baadaye, mara anakuja mteja na bei nzuri unamuuzia anasafirisha kwenda mjini.
Yakifika huko yanasagwa dona hata bila kusafishwa mwishowe mnakula sumu mbichi kabisa ambayo hata wadudu wasingeigusa.
Tunaishi kwa neema ya Mungu tu ila tunakula sumu kabisa.
Miaka ya hivi karibuni kumezuka viwanda vingi sana mitaani vinavyosaga unga wa mahindi na muhogo, ubora wa unga huo u atia mashaka kwani viwanda husika haviko kwenye usafi unaoridhisha.
Kiwanda ambacho hakiko kwenye usafi hata ubora wa unga wake utatia shaka, ni wazi viwanda hivyo vina mashine ya kukoboa na kusaga, havina mashine ya kusafisha nafaka husika hivyo kunauwezekano mkubwa kusagwa na takataka nyingine.
Nafaka zinazopatikana miaka hii huwa na uwezekano wa kuathirika na sumu kuvu na sumu zitokanazo na madawa ya kuhifadhia nafaka pamoja na ya kuua wadudu mashambani, haya yote ni hatari kwa afya zetu.
Ni jambo lililo wazi nchini kwetu hakuna utamaduni wa kichukua sampuli madukani na kwenda kuzipima maabara, TBS na TFDA nendeni madukani mchukue sampuli mkazipime naamini matokeo yatalishitua taifa kutokana na utitiri wa viwanda vya vichochoroni.
Hiyo sembe na dona ndiyo tunazozizungumzia, vyote vina sumu na waliopewa jukumu kudhibiti hawana habari.Nailinda familia yangu kwa kununua mahindi wakati wa mavuno kutoka kwa mkulima ninayemfahamu kisha nayakausha vizuri juani nayahifadhi kwenye mifuko ya PCS. Nasaga dona Kila ninapohitaji.
ninapokuwa mbali na nyumbani wakati wa kula lazima nile wali au ugali wa sembe.
Hili ni Kweli kabisaMiaka ya hivi karibuni kumezuka viwanda vingi sana mitaani vinavyosaga unga wa mahindi na muhogo, ubora wa unga huo u atia mashaka kwani viwanda husika haviko kwenye usafi unaoridhisha.
Kiwanda ambacho hakiko kwenye usafi hata ubora wa unga wake utatia shaka, ni wazi viwanda hivyo vina mashine ya kukoboa na kusaga, havina mashine ya kusafisha nafaka husika hivyo kunauwezekano mkubwa kusagwa na takataka nyingine.
Nafaka zinazopatikana miaka hii huwa na uwezekano wa kuathirika na sumu kuvu na sumu zitokanazo na madawa ya kuhifadhia nafaka pamoja na ya kuua wadudu mashambani, haya yote ni hatari kwa afya zetu.
Ni jambo lililo wazi nchini kwetu hakuna utamaduni wa kichukua sampuli madukani na kwenda kuzipima maabara, TBS na TFDA nendeni madukani mchukue sampuli mkazipime naamini matokeo yatalishitua taifa kutokana na utitiri wa viwanda vya vichochoroni.
Hilo unalolisema halina ubishi kwani ndiyo moja ya jukumu lao, chini ya usagaji holela vichochoroni hawawezi kulitekeleza jukumu hilo, ukiwa na mashine ya kusaga nunua mahindi yasage kama yalivyo, weka kwenye mifuko kisha uza, hakuna shida.Mkuu kwa uelewa wangu TBS pamoja na taasisi ya chakula na lishe (TFNC) kwa kushirikiana na taasisi binafsi pamoja na za serekali (Tamisemi, afya, kilimo, Mkemia mkuu, waziri mkuu) huwa na zoezi la ufuatiliaji wa usalama wa vyakula lakini pia na urutubishwaji wa hivi vyakula (food safety and fortification assessment) ambapo sampuli huchukuliwa viwandani (mathalani unga wa ngano kwa Bakhressa au sembe hapo tandale kwa wasagaji wadogo au mafuta ya alizeti pale dodoma na kwingineko nchi nzima) sampuli pia huchukuliwa sokoni zinapouzwa (madukani, supermarket,kiosk kwa mangi nk). Sampuli hizi hupelekwa kupimwa kwenye maabara zetu za ndani (tbs,tfnc na mkemia mkuu) lakini pia baadhi hupelekwa maabara za nje ambazo huitwa reference labs.sasa majibu ya huu uchunguzi hurudishwa kwa mamlaka husika kwa ajili ya utekelezaji (kwa kiwango gani utekelezaji unafanyika sijui).
Pascal MayallaRais Samia atakuwa Moshi na moja ya mambo atakayo yafanya ni suala la chakula na lishe, Paskali Mayalla yuko huko na Rais Samia atafika uwanja wa Pasua, nategemea Paskali ataiwakilisha JF kufikisha ujumbe huu.
Kama amefikia kwenye hoteli ya kitalii ataona halimuhusu ila atakaporudi huku atakumbuka, lakini ninamuamini sana.
Wasisahau na hawa Wauza unga lishe. Sasa hivi unga unamchanganyiko hadi midizi ya Kitarasa, kweme, Beet root, Karoti, nyanya, rozella, mlonge etc. Tbs, tfda Njooni twafa hukuMiaka ya hivi karibuni kumezuka viwanda vingi sana mitaani vinavyosaga unga wa mahindi na muhogo, ubora wa unga huo u atia mashaka kwani viwanda husika haviko kwenye usafi unaoridhisha.