TBS na TFDA okoeni maisha yetu kwa kupima ubora wa unga wa mahindi na muhogo unaosagwa mitaani

Nailinda familia yangu kwa kununua mahindi wakati wa mavuno kutoka kwa mkulima ninayemfahamu kisha nayakausha vizuri juani nayahifadhi kwenye mifuko ya PCS. Nasaga dona Kila ninapohitaji.

ninapokuwa mbali na nyumbani wakati wa kula lazima nile wali au ugali wa sembe.
 
Ndiyo hivyo mkuu
 
TBS na TFDA kazi kubwa wanayo fanya ni kwenda kuuza sura kwenye maonesho ya sabasaba na mengineyo. Hata ukiwaona kwenye tv ni pale wanapo shika vipodozi na viwatilifu kwenye viduka. Bidhaa nyingi ziingizwazo na kuzalishwa nchini ni mbovu na hata washikwao huishia kuelewana.
 
Unakuta umepiga mahindi dawa ili uhifadhi kwa matumizi ya baadaye, mara anakuja mteja na bei nzuri unamuuzia anasafirisha kwenda mjini.

Yakifika huko yanasagwa dona hata bila kusafishwa mwishowe mnakula sumu mbichi kabisa ambayo hata wadudu wasingeigusa.

Tunaishi kwa neema ya Mungu tu ila tunakula sumu kabisa.
 
Hili la sumu kwenye nafaka hivi sasa ni tatizo kubwa sana huku wanaotakiwa kudbibiti wanalipuuzia kama vile hakuna tatizo!
 
Kwa kweli madawa yanayohifadhi nafaka ikiwemo mahindi ni salama kwa afya jamani?
 
Tuwajibike wenyewe kuliko kusubir hzo mamlaka. Sidhan kama itatokea TFDA or TMDA Kufanya operesheni ya kucheki bidhaa duka kwa duka...
Hata vipodoz vilivyozuiliwa kutumika (vyenye hydroquinone, sulphur n.k) bd vipo madukan na vinauzika kama kawaida.
 
Mkuu kwa uelewa wangu TBS pamoja na taasisi ya chakula na lishe (TFNC) kwa kushirikiana na taasisi binafsi pamoja na za serekali (Tamisemi, afya, kilimo, Mkemia mkuu, waziri mkuu) huwa na zoezi la ufuatiliaji wa usalama wa vyakula lakini pia na urutubishwaji wa hivi vyakula (food safety and fortification assessment) ambapo sampuli huchukuliwa viwandani (mathalani unga wa ngano kwa Bakhressa au sembe hapo tandale kwa wasagaji wadogo au mafuta ya alizeti pale dodoma na kwingineko nchi nzima) sampuli pia huchukuliwa sokoni zinapouzwa (madukani, supermarket,kiosk kwa mangi nk). Sampuli hizi hupelekwa kupimwa kwenye maabara zetu za ndani (tbs,tfnc na mkemia mkuu) lakini pia baadhi hupelekwa maabara za nje ambazo huitwa reference labs.sasa majibu ya huu uchunguzi hurudishwa kwa mamlaka husika kwa ajili ya utekelezaji (kwa kiwango gani utekelezaji unafanyika sijui).
 
Upo sahihi, inatakiwa hao watu wanaofanya biashara ya ku pack unga wapime kila batch wanayotengeneza kuingiza sokoni. Nafikiri hili lisisitizwe zaidi kwa wanao pack dona kuliko sembe hasa linapokuja swala la kuangalia kiwango cha sumu kuvu (aflatoxin). Pia kumekuwepo na trend ya kusaga karanga kutengeneza peanut butter, hii nayo ni ya kuangalia kwa sababu kama ilivyo dona karanga na zenyewe zinaweza kuwa na kiwango kikubwa sana cha aflatoxin.​
 
Hiyo sembe na dona ndiyo tunazozizungumzia, vyote vina sumu na waliopewa jukumu kudhibiti hawana habari.
 
Hili ni Kweli kabisa
 
Hilo unalolisema halina ubishi kwani ndiyo moja ya jukumu lao, chini ya usagaji holela vichochoroni hawawezi kulitekeleza jukumu hilo, ukiwa na mashine ya kusaga nunua mahindi yasage kama yalivyo, weka kwenye mifuko kisha uza, hakuna shida.
Ukiwauliza TBS watakuambia wanapima lakini hali halisi hawapimi na hata wanaosaga hawawajui wako wapi! Tunakufa taratibu.
 
Rais Samia atakuwa Moshi na moja ya mambo atakayo yafanya ni suala la chakula na lishe, Paskali Mayalla yuko huko na Rais Samia atafika uwanja wa Pasua, nategemea Paskali ataiwakilisha JF kufikisha ujumbe huu.
 
Watanzania wanakula sumu kila siku..sio kwenye dona tu...ni muda wa kujilinda ukisubiri TBS itakua umechelewa..taasisi zetu ninza upogaji zaidi sio utendaji.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wiki imeisha naomboleza vifo vya mbwa wangu kwa kula dona.
Sjui na nyie mnaopenda ugali wa dona unaovunda madukani na kugeuka sumu hatari kabisa!..
Km mbwa walitapika dam na kuharisha damu ni hatari sana.
 
Wasisahau na hawa Wauza unga lishe. Sasa hivi unga unamchanganyiko hadi midizi ya Kitarasa, kweme, Beet root, Karoti, nyanya, rozella, mlonge etc. Tbs, tfda Njooni twafa huku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…