TBS YAWATAKA WAFANYABIASHARA WA BIDHAA ZA VIPODOZI NA CHAKULA PAMOJA NA MAJENGO YA KUHIFADHIA NA KUUZIA BIDHAA HIZO KUJISAJILI KIELEKTRONIKI
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) leo Tarehe 22 Agosti, 2022 imewataka wafanyabiashara wa Chakula na Vipodozi pamoja na wamiliki wa Majengo yanayotumia katika kuhifadhia na kuuzia bidhaa za Chakula na Vipodozi KUJISAJILI katika mfumo wa kielektroniki hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa usajili wa bidhaa na Majengo kutoka TBS katika Mkutano na Waandishi wa habari leo Makao Makuu ya TBS, Ubungo Dar es salaam.
Kaimu Meneja wa usajili wa bidhaa na Majengo Bi. Gwantwa Mwakipesile amesema "sisi kama TBS tunajukumu kubwa sana la kulinda usalama wa mtumiaji wa bidhaa za vipodozi na Chakula kwa kudhibiti uingizaji wa bidhaa Nchini zisizokidhi takwa la ubora na Viwango"
Mfumo wa usajili unasaidia kwa kiasi kikubwa katika kudhibiti bidhaa feki na zisizokuwa na ubora Nchini lengo likiwa kulinda usalama wa mtumiaji wa bidhaa hizo.
"Kwa sasa TBS tunatumia mfumo wa kielektroniki (OAS) katika husajili wa Majengo, Vipodozi pamoja na bidhaa za Chakula hivyo wafanyabiashara wanaweza kutembelea tovuti ya TBS (www.tbs.go.tz) kwa ajili ya kusajili" - Bi.Gwanta Mwakipesile.
Mfumo huo unamtaka Mfanyabiashara kusajili bidhaa za vipodozi na Chakula kabla ya kuviingiza Nchini kwa ajili ya matumizi.
Bi. Mbumi Mwampeta Afisa kudhibiti ubora TBS amesema " mara baada ya mfanyabiashara kusajili bidhaa yake ya Vipodozi atapatiwa Cheti na atakiwa kuhuwisha Cheti hicho kila baada ya miaka Mkutano (5) hivyo niwaombe wafanyabiashara wote wa Vipodozi Nchini kutembelea tovuti ya TBS kwa kuanza taratibu za usajili maana ni takwa la kisheria"
Mwisho TBS inawataka wafanyabiashara wa Vipodozi na Chakula pamoja na wamiliki wa Majengo ya kuhifadhia na kuuzia bidhaa hizo KUJISAJILI na Kupata Cheti ili kuondokana na usumbufu unaoweza kujitokeza wakati wa uingizaji bidhaa za vipodozi na Chakula nchini.