TBS yakamata Mabati 125,280 yasiyokidhi viwango, zoezi la kuyateketeza laingia doa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
deb5406e-fa51-43b6-b614-eea3362d814c.jpg

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeiandikia barua kampuni ya uagizaji na usambazaji wa mabati nchini URHOME Company Limited kuhakikisha ndani ya siku tatu imewapatia taarifa ya mabati 2176 kati 125,280 baada ya kufanyiwa ukaguzi na kugundulika hayajakidhi viwango.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 30, 2022 Jijini Dar es Salaam, Meneja wa uthibiti wa Shehena zinazoingia na kutoka nchini Mhandisi Saidi Mkwawa amesema Kampuni hiyo baada ya kuingiza nchini mabati hayo, TBS ilichukua sampuli na kuzipeleka kwenye maabara ya Shirika ili kubaini kama zimeweza kukidhi viwango stahiki kwa mujibu wa sheria.

Aidha, baada ya matokeo ya uchunguzi ilibainika kwamba mabati kutoka kampuni hiyo yameshindwa kukidhi viwango vya ubora vilivyotarajiwa, kama ilivyo taratibu za sheria, kulikuwa na njia mbili aidha kurudisha au kuteketeza na mteja alikubaliana na njia ya kuteketeza na zoezi la uteketezaji lilianza.

"Wakati tukiendelea kuteketeza ambapo mabati hayo awali yalikuwa 125,280 tukaja tukabaini mabati 2,176 hayapo na taratibu za kisheria zimeshaanza," amesema.

Pamoja na hayo Mhandisi Mkwawa amesema watahakikisha mabati yote yanapatikana na zoezi la uteketezaji litaendelea sambamba na mengine.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, David Ndibalema amewahimiza wafanyabiashara na waingizaji wabidhaa kutumia vizuri vibali vya masharti kwa kuhakikisha wanazingatia yale masharti ambayo yamewekwa wakati wa kutoa vibali hivyo.

Masharti yenyewe ni kwamba kama mzigo bado upo chini ya uchunguzi mzigo huo hautakiwi usambazwe, kuuzwa au kutumiwa kwa njia yoyote ile na tutaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa wale ambao wanakiuka akiwemo huyu ambaye ameingiza huu mzigo wa mabati ambayo yamegundulika yapo chini ya viwango

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara, Christopher Mramba amesema wamesikitishwa na tukio hilo na kukemea ukiukwaji wa masharti ya vibali vinavyowekwa na serikali na kuzingatia sheria na kuendelea kujenga utamaduni wakuzingatia masharti ya ubora wa bidhaa na kamwe serikali haitaacha soko la Tanzania liwe dampo kuweka bidhaa zisizo na ubora.

"Tutaendelea kushirikiana na vyombo vya Serikali kufuatilia bidhaa ambazo zimeingia sokoni kinyume na sheria na kuchukua hatua stahiki za kisheria na nitoe wito kwa wafanyabiashara wote nchini kuzingatia uaminifu na matumizi mazuri ya fursa zinazotolewa na serikali za kuweka mazingira wezeshi ya biashara ikiwemo hii fursa ya kutoa kibali cha masharti maalumu ya kutoa mzigo bandarini ili bandari yetu iendelee kuwa na ufanisi unaotakiwa na pasiwe na msongamano ili biashara nyingine ziwezee kufanyika," amesema
 
TBS YAZUIA SHEHENA YA MABATI YALIYO CHINI YA KIWANGO

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) leo Tarehe 30 Septemba, 2022 imetembelea na kujionea Shehena ya Mabati yaliyo chini ya kiwango yaliyozuiliwa na TBS kwa matumizi hapa Nchini.

TBS Kupitia Kaimu Mkurugenzi Mkuu(TBS) Bw. David Ndibalema akiongea na Waandishi wa habari alipotembelea ghala la Kampuni ya URHOME inayoagiza na kusambaza bidhaa za Mabati Nchini kutoka Nchini China na kukuta Shehena ya Mabati yaliyo chini ya kiwango.

Bw. Ndibalema alitoa onto kwa wafanyabiashara hao baada ya kukiuka taratibu zilizowekwa na TBS na kusema kuwa hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

"Ndugu wafanyabiashara tukumbuke lengo la TBS ni kuhakikisha mlaji wa mwisho anapata bidhaa bora na zenye Viwango pamoja na kuwezesha biashara Nchini kufanyika kwa kuzingatia ubora uliowekwa" - Bw. Ndibalema.

Pia Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara kutoka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Christopher Mramba amekagua Mabati hayo yaliyo chini ya kiwango Mali ya Kampuni ya URHOME yaliyo zuiwa na TBS kwa ajili ya uteketezaji, Mabati hayo yapo maeneo ya Kwa Sokota Wilayani Temeke, Dar es salaam.

Mramba amewahasa wafanyabiashara kufuata taratibu zinazowekwa ili kuepuka usumbufu na gharama.

"Ikumbukwe lengo la serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona biashara Nchini Zinastawi sambamba na kufuata taratibu na Sheria zilizowekwa ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza" - Alisema Bwana Mramba wakati wa mkutano na waandishi wa habari ghalani hapo.
 
Attachments

  • 20220930_165737.jpg
    20220930_165737.jpg
    34.3 KB · Views: 9
  • 20220930_165731.jpg
    20220930_165731.jpg
    42.8 KB · Views: 7
  • 20220930_165725.jpg
    20220930_165725.jpg
    360.3 KB · Views: 8
  • IMG-20220930-WA0100.jpg
    IMG-20220930-WA0100.jpg
    60.4 KB · Views: 7
  • IMG-20220930-WA0103.jpg
    IMG-20220930-WA0103.jpg
    58.2 KB · Views: 8
  • IMG-20220930-WA0102.jpg
    IMG-20220930-WA0102.jpg
    62.8 KB · Views: 8
  • IMG-20220930-WA0104.jpg
    IMG-20220930-WA0104.jpg
    63.7 KB · Views: 9
  • 20220930_165656.jpg
    20220930_165656.jpg
    163.8 KB · Views: 10
  • 20220930_165701.jpg
    20220930_165701.jpg
    198.4 KB · Views: 9
  • 20220930_165708.jpg
    20220930_165708.jpg
    325.6 KB · Views: 11
View attachment 2372777
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeiandikia barua kampuni ya uagizaji na usambazaji wa mabati nchini URHOME Company Limited kuhakikisha ndani ya siku tatu imewapatia taarifa ya mabati 2176 kati 125,280 baada ya kufanyiwa ukaguzi na kugundulika hayajakidhi viwango.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 30, 2022 Jijini Dar es Salaam, Meneja wa uthibiti wa Shehena zinazoingia na kutoka nchini Mhandisi Saidi Mkwawa amesema Kampuni hiyo baada ya kuingiza nchini mabati hayo, TBS ilichukua sampuli na kuzipeleka kwenye maabara ya Shirika ili kubaini kama zimeweza kukidhi viwango stahiki kwa mujibu wa sheria.

Aidha, baada ya matokeo ya uchunguzi ilibainika kwamba mabati kutoka kampuni hiyo yameshindwa kukidhi viwango vya ubora vilivyotarajiwa, kama ilivyo taratibu za sheria, kulikuwa na njia mbili aidha kurudisha au kuteketeza na mteja alikubaliana na njia ya kuteketeza na zoezi la uteketezaji lilianza.

"Wakati tukiendelea kuteketeza ambapo mabati hayo awali yalikuwa 125,280 tukaja tukabaini mabati 2,176 hayapo na taratibu za kisheria zimeshaanza," amesema.

Pamoja na hayo Mhandisi Mkwawa amesema watahakikisha mabati yote yanapatikana na zoezi la uteketezaji litaendelea sambamba na mengine.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, David Ndibalema amewahimiza wafanyabiashara na waingizaji wabidhaa kutumia vizuri vibali vya masharti kwa kuhakikisha wanazingatia yale masharti ambayo yamewekwa wakati wa kutoa vibali hivyo.

Masharti yenyewe ni kwamba kama mzigo bado upo chini ya uchunguzi mzigo huo hautakiwi usambazwe, kuuzwa au kutumiwa kwa njia yoyote ile na tutaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa wale ambao wanakiuka akiwemo huyu ambaye ameingiza huu mzigo wa mabati ambayo yamegundulika yapo chini ya viwango

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara, Christopher Mramba amesema wamesikitishwa na tukio hilo na kukemea ukiukwaji wa masharti ya vibali vinavyowekwa na serikali na kuzingatia sheria na kuendelea kujenga utamaduni wakuzingatia masharti ya ubora wa bidhaa na kamwe serikali haitaacha soko la Tanzania liwe dampo kuweka bidhaa zisizo na ubora.

"Tutaendelea kushirikiana na vyombo vya Serikali kufuatilia bidhaa ambazo zimeingia sokoni kinyume na sheria na kuchukua hatua stahiki za kisheria na nitoe wito kwa wafanyabiashara wote nchini kuzingatia uaminifu na matumizi mazuri ya fursa zinazotolewa na serikali za kuweka mazingira wezeshi ya biashara ikiwemo hii fursa ya kutoa kibali cha masharti maalumu ya kutoa mzigo bandarini ili bandari yetu iendelee kuwa na ufanisi unaotakiwa na pasiwe na msongamano ili biashara nyingine ziwezee kufanyika," amesema
Leo imekuwaje? TBS ni wala rushwa wakubwa sana!! sasa hivi kuna bati za hovyo kabisa madukani. Leo ndo wamekumbuka? Au mama kawaruhusu?
 
Shida ni kwamba ukaguzi unafanyika leo, majibu yanatoka baada ya miaka miwili...
 
SI Bora yagaiwe vijijini huko watu wenye nyasi waezeke
 
Kuna mamilioni ya watanzania wanalala kwenye vibanda vya nyasi, mabati yaliyochakaa na kujaza kutu nk. Busara itumike, wapewe TASAF wakasaidie kaya maskini sana huko vijijini. Heri kidogo/dhaifu kuliko kukosa kabisa.
 
Hivi viwanda kibao ambavyo vinatengeneza mabati substandard mbona hawavigusi?
 
Back
Top Bottom