sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Leo ni thursday (alhamisi) sio mbaya kukumbushia kidogo mambo kadhaa, tbt throwbak thursaday.
2011 nilikuwa nimemaliza form six nikiwa na miaka 20,
Mitihani tumemaliza mwezi wa pili, vyuo tunaingia october, hapo nina miezi 8 yani.
Warembo napishana nao mtaani, naishia tu kuwapa hi, nimefulia ile mbovu mbaya aisee.
Kiukweli nilikuwa natamani sana warembo, sasa nikaanza kujiuliza hapa ntawezaje, baada ya kutafakari nikaona hakuna ujanja njia rahisi ni pesa.
Nikiwa nina elimu ya somo la uchumi kama mhitimu qa form 6, nikapitia pitia vitabu vya Ambilikile, nikaona kuna sehemu aligusia kwamba nchi ikiwa katika anguko la kiuchumi ama kuprint pesa nyingi basi si ajabu pesa hio kukosa thamani na watu kuanza kununua mikate kwa bilioni, Ni kama kile kilichotokea Zimbabwe watu walikuwa wana noti nyingi ila dukani huwezi nunua hata soda maana pesa haina thamani.
Sasa kuna hawa jamaa huwa wananunua pesa mitaani sana sana za zamani, moja wao alikuwa rafiki yangu, umri alikuwa na 32 hivi, nilimpa elf 14, baada ya wiki akanikabidhi maburungutu matatu ya noti mpya zikiwa ndani ya rambo, Kuna siku nilienxa mjini kufatilia ni za nchi gani ila nilipofika sehemu ya kubadilishia pesa (bureau de change) hawakuitambua, ni aidha ilikuwa ya zamani au ya nchi wasiyoijua
Sasa mchezo wangu ukawa nikikutana na binti kanivutia, namwomba tuongee pembeni, akinipa namba natoa waleti imetuna balaa, naifungu kwa sifa nae aone minoti, alafu nasingizia nina elf 2 tu ya Tanzania, aichukue ya vocha.
Wee!! wee! wee! walikuwa wananipaparikia nikiwapigia au kuwa text acha kabisa, hapo washazuzuka na minoti feki.
Basi hapo ntaingizia vocal zangu kwamba nina mda mchache kukaa huu mkoa na nimempenda na namsifia uwongo kwamba ana akili ya kuanzisha biashara ntamsaidia mtaji milion 2, kashazuzuka hapo.
Aisee!! nlizitafuna sana jamani!!, wengi walinizidi tena wengi walikuwa ni 23, 24 na 25 basi na ule ushamba wangu nikawa najiona nipo juu kisa nmelala na mtu aloenizidi umri
Yani ilikuwa mfukoni ni kubeba mpira na wallet iliyotuna.