TBT: Mwaka 1985 Scotland Yard walikuja Tanzania kuchunguza BOT na 1990 walikuja Kenya kifo cha Waziri Dr Robert Ouko

TBT: Mwaka 1985 Scotland Yard walikuja Tanzania kuchunguza BOT na 1990 walikuja Kenya kifo cha Waziri Dr Robert Ouko

Matukio ya utekaji yapo mengi na mengine wahusika mbona walidakwa vizuri tu mfano wa karibuni ni mtoto Albino aliyetekwa na kuuawa kule Geita watekaji na wauaji akiwemo padri na baba mzazi wa mtoto walidakwa

Pia kuna mfanyakazi wa mgodi wa Geita aliuawa na wasiojulikana mbons walidakwa wote na kuhukumiwa kunyongwa

Kesi ingine ya mfanyabiashara huko Songea kutekwa na kuporwa pesa na kuuawa na kutupwa porini mbona wahusika walidakwa na polisi Dodoma na wako mikononi mwao
Vipi MO dewji, Lissu, Roma, N.k.
 
Asante kwa kuchangia mada.

Kuhusu polisi wetu kuanza uchunguzi je hili ni tukio kwanza? Si la jana wala leo wala mwaka jana wala mwaka juzi.

Tukubali tusaidiwe na pia tupate uzoefu kwa wenzetu
Tanzania iko vizuri kwa taarifa yako inaaminiwa kimataifa kwenye upelelezi

Aliyelipua ubalozi wa marekani Tanzania vyombo vyote vya kimataifa vya upelelezi vilishindwa kumpata .Tanzania ndio walifanikuwa kumdaka nje ya nchi na kuwakabidhi marekani
 
Tanzania iko vizuri kwa taarifa yako inaaminiwa kimataifa kwenye upelelezi

Aliyelipua ubalozi wa marekani Tanzania vyombo vyote vya kimataifa vya upelelezi vilishindwa kumpata .Tanzania ndio walifanikuwa kumdaka nje ya nchi na kuwakabidhi marekani
Aliyelipua Imma Advocates je?
 
Vipi MO dewji, Lissu, Roma, N.k.
Wengine hapo walikataa kutoa ushirikiano na polisi kuwa hawataki polisi wa Tanzania washughulikie ulitakaje sasa? Mfano Lisu aliambiwa apeleke Dereva wake ahojiwe akagoma kumpeleka polisi

Sasa mtu hataki kutoa ushirikiano na polisi ,polisi wafanyaje wao kwa utaalamu wao wanasema tunamtaka huyu aje asaidie upelelezi mtu hataki
 
Wengine hapo walikataa kutoa ushirikiano na polisi kuwa hawataki polisi wa Tanzania washughulikie ulitakaje sasa? Mfano Lisu aliambiwa apeleke Dereva wake ahojiwe akagoma kumpeleka polisi

Sasa mtu hataki kutoa ushirikiano na polisi ,polisi wafanyaje wao kwa utaalamu wao wanasema tunamtaka huyu sje asaidie upelelezi mtu hataki
Hahaa sawa.
 
Tujikumbushe matukio muhimu yaliyotokea hapo awali ktk nchu yetu na majirani zetu Pia.

Pamoja na mambo mengi yanayozungumzwa kuhusu msala huu wa Utekaji, utesaji, upoteaji na mauwaji ya Raia ambayo yameshika kasi ktk nyakati hizi ni wazi sasa tunaweza kuswma yafuatayo.

1. Mh Rais Amiri Jeshi Mkuu amethibitisha mpaka sasa hajawajua wanaohusika na matuko labda mpaka uchunguzi ufanyike na apewe ripoti kama alivyoagiza.
2. Mahakama haiwajui wahusika
3. Bunge haliwajui wahusika.
4. Jeshi la Polisi Tanzania bado haliwajuia wahusika.
5. Vyombo vingine vya ulinzi na usalama pia haviwajui wahusika.
6. Wananchi nao kwa wingi wao 60M hakuna anyewajua hao watekaji na wauwaji hivyo hofu imetanda kila mahali.
Kwa kusema hivyo ndio maana tunasema tunahitaji vyombo vyenye uwezo mkubwa na uzoefu na uaminifu usio na chembe ya shaka kutusaidia kuchunguza zahama hii inatotukabili kama Taifa.

Katika orodha ya Sheria zetu za Nchi hakuna mahali Sheria wala kanuni inazuia Kuomba vyombo au kushirikiana na vyombo vingine vya kimataifa kufanya uchunguzi kwenye uharifu ndani ya Nchi.

Kwani haitakuwa mara ya kwanza kufanya hivyo na pengine inaweza kuzidisha mahusiano na kujange uwezo kwenye vyombo vya ndani kiutalamu na uchunguzi.

Mwaka 1984 muda wa asubuhi Jengo la BOT pale ufukweni Dar es salaam llilishuhudiwa na maelfu ya watu likiteketea kwa moto, vyombo vya ulinzi na usalama viliorganize na kuhakikisha usalam na ulinzi mkali unawekwa ili kuhakikisha hakuna uharibifu unajitokeza wakati wa janga. Hata hivyo chanzo cha moto na madhara yake hayakufahamika mpaka Pale Serikali ililazimika kuomba msaada kwa Jeshi la Polisi la Uingereza, Scotland Yard.

Scotland Yard ni Kitengo Mahususi cha Jeshi la Polisi la Uingereza kilichobobea kwenye maswala ya kiuchunguzi ya uharifu wa kimataifa( internationa Organize crime Investigation section). Kinafahamika kama kikosi imara duniani kote kwenye maswala ya forensiki.

Pia wakati wa Utawala wa Daniel Arap Moi, Rais Wa pili wa kenya kilitokea kifo baada ya mauwaji ya Waziri wake wa Mambo ya Nje Dr Robert Ouko. Serikali ya Kenya ilikazimu kuwaita Team ya Scotland yard ikiongozwa na Kachero, Detective Super Intendent John Troon na wenzake wawili February 1990.

Kifo cha Dr Robert Ouko kilitokea miaka michache baada ya kupata misuko suko kutokana na hulka yake ya kukosoa utawala wa Kidikiteta wa Rais Moi ambapo kabla ya kifo chake alifunguliwa mashtaka mahakamani na akaamua Kujiuzulu baada ya kesi kuisha kati ya mwaka 1982 na 1985.

Report ya Uchunguzi ya Kifo cha Robert Ouko iliwekwa wazi na Wakenya wote wanapata fursa ya kuisoma na kuujua ukweli wa kile kilichojiri.

Soma Pia: Freeman Mbowe: Scotland Yard ya Uingereza ichunguze Matukio ya Utekaji na Uuaji nchini

Hivyo hatuna sababu ya kusua sua kufanya haraka kama kweli tuna nia ya dhati ya kukomesha matukio haya.
Watekaji wetu ni hodari sana, sizani kama jamaa watamaliza kazi yao kabla na wao awajatekwa.
 
Mkuu; Mimi Quotation yangu ya moto ni kuhusu BOT kama ulivyoandika. Ndio nikaulzia ripoti ya Scotlandyard. Hebu ipitie vzuri halafu nasubiri jibu
Okay sawa.....baadhi ya vyanzo vya habari zilivyozungumzia swala hilo ikiwemo Global Publishers wanasema Baada ya uchunguzi huo Repoti ya Scotland yard haikuwekwa wazi.
 
Back
Top Bottom