Feld Marshal Tantawi
JF-Expert Member
- Dec 24, 2014
- 655
- 1,069
CHAMA cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Dodoma, kimesema japo serikali haijawafungia watu ndani, lakini hali ya biashara mkoani hapa imeendelea kuwa mbaya siku hadi siku.
Akizungumza wakati wa mahojiano na Habari- LEO, Mwenyekiti wa TCCIA mkoani hapa, Denis Nyabiri amesema katika utafiti mdogo alioufanya kwa wanachama wake mkoani hapa, amegundua kuwa hali ya biashara siyo nzuri.
Alisema kila mfanyabiashàra mjini na vijijini, analalamika biashara kuwa mbaya, japo tangu awali hali haikuwa nzuri lakini kwa sasa imezidi kuwa mbaya.
“Nataka ufanyike utafiti kuhusu hali ya biashara nchini kwa sababu hata kama serikali haijawazuia watu ndani lakini hali imekuwa mbaya sijui kwa sababu serikali imezuia mikusanyiko na safari zisizo za lazima?”vip maeneo mengine huko hali ipoje?