TCD endapo mtaelewa kauli aliyoitoa George (Mkenya) mtatambua hakuna Tume bila Katiba na hakuna Katiba bila Tume Huru

TCD endapo mtaelewa kauli aliyoitoa George (Mkenya) mtatambua hakuna Tume bila Katiba na hakuna Katiba bila Tume Huru

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
George amewaeleza wananchi mambo muhimu sana ambayo kwa historia ya Kenya kwenye mchakato wa Katiba hakuna tofauti na Tanzania.

Kenya walikusanya maoni ya wananchi then chama tawala na Serikali wakayakataa hayo maoni yaliyokuwa na jina la BOMAS. Chama tawala wakaanzisha mchakato wao na kuipeleka hadi kwa wananchi ukakatali. Baada ya kukataliwa ikasababisha vita mwaka 2007 ambapo watu walipoteza maisha na haya yalikuwa matokeo ya ufa uliojengwa na Serikali na chama tawala.

Baadaye ikawalazimu kutafuta wasuluhishi wa kimataifa wakiweno akina Koffi Annan na Tanzania ikiwa mstari wa mbele. Wasuluhishi wakawarejesha kwenye katiba na kushauri iundwe timu ya watu wachache experts wapitie mchakato wote na kushauri.

Timu hiyo ikaundwa na raia wa Kigeni watatu na Wakenya sita jumla watu tisa. Kazi kubwa ikawa kuangalia ni mambo gani yanabishaniwa na yapi hayana utata. Wakamaliza kazi wakasawazisha ndipo ikapatikana katiba Mpya ya Kenya.

Kwa upande wa Tanzania mtakumbuka baada ya rasimu ya Warioba Bunge liliondoa maoni ya wananchi na kuweka maoni ya chama tawala na Serikali. Kwa wanaofahamu mchakato ule ulimwondoa Mwanasheria Mkuu Zanzibar ofisini kwa sababu tu alisimama na maoni ya wananchi. Baada ya bunge kupitisha rasimu ilitakiwa iende kupigiwa kura lakini JK akaangalia upepo akatambua hakuna mwananchi wakuipitisha katiba ya chama akaweka mpira kwapani.

Mwaka mmoja baadaye ukaingia utawala amabo kwao si katiba mpya TU Bali hata Ile iliyopigiwa kelele waliivunja. Mwamba alipoingia akaanza na wapinzani kisha akarejesha kichapo kwa wale wale waliokwamisha mchakato wa Katiba na baadhi yao may be awapo Duniani Kwa frastrustaion walizopata. Akateua na kuweka watu anavyojisikia huku wale walioumizwa wakijua kabisa endapo wangekubaliana na rasimu ya Warioba na katiba ikabadilishwa wasingekuwa wanatenguliwa usiku na mchana , asingeitwa wahujumu uchumi Kwa sababu tu wamemzidi mwenzao nguvu ya kiuchumi au kisiasa. Mahakama may be ingekuwa huru na dhamana ingekuwa wazi. Baada ya kujuta Kwa muda na kumkumbuka Mzee waryoba Leo watu wale wale ndio wanasema hakuna haja ya Katiba mpya...

Mzee Warioba amewahoji watu ahawa wanatoa wapi mamlaka ya kuondoa mambo ya muungano bila kubadili katiba? Maana yake anawakumbusha wanavunja sheria.

Kwa maneno ya George, ni wazi Tanzania kupata katiba inahitaji watu neutral na watu wachache. Leo tunapowaza referendum tunategemea Tume Gani inakwenda kusimamia? Tunapowaza kuwa na Tume huru tujiulize hiyo Tume huru inaundwa na akina nani na Kwa maslahi Gani wakati hakuna sheria inayomakataza Rais kuteua wajumbe atakotaka?

Mwisho, kama TCD imeshindwa kuheshimu maamuzi ya CHadema kutoshiriki mkutano wao itaweza kumkatalia Mhe. Rais uundaji wa tume?
 
Asante kwa kuwajiza TCD, Ila.kwa.kuku walizojaza mezani.leo wakitumbua sijui kamawatakusikia
 
Back
Top Bottom