TCHOUKBALL ni mchezo gani ?

TCHOUKBALL ni mchezo gani ?

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
TCHOUKBALL kama unavyotamka chukboli ni moja kati ya michezo inayozidi kuchukua nafasi ya umaarufu duniani.
Mchezo huu ambao kwa sasa umefika Tanzania na tayari ndani ya Arusha mchakato wa kutengeneza timu umeshaanza baada ya vijana wachache walobahatika kujifunza mchezo huo kuanza kuunda timu.
Mchezo huu wa tchoukball ulianza kutambulishwa rasmi mwaka 1970 na mtu aliejulikana kwa jina la Dk Hermann Brandt ambapo mpaka sasa mataifa mengi yameufahamu mchezo huo.
tchoukball ni mchezo ambao unachezwa ktk uwanja mdogo na wenye magoli mawili madogo.
Mchezo huu huchezwa kwa mikono na upo tofauti kabisa na mpira wa miguu au handball tuloizoea kwani ktk mchezo wa tchoukball hakuna kukabana kama ilivyo ktk mpira wa miguu na hivyo mchezo huo kuitwa kwa jina la peace game kwa huitaji kumzuia mwenzako wakati anapotaka kufunga goli.

FAIDA ZA TCHOUKBALL .
Kama ilivyo kwa michezo mingine tchoukball ni mchezo wenye kuwakutanisha watu wa aina mbalimbali,mataifa tofauti na rangi tofauti.
Mchezo huu huwaunganisha watu pamoja na kujenga urafiki,ujamaa na undugu wa kweli.
tchoukball humjenga mchezaji katika afya ya akili na kupanua ubongo na maarifa yake.
Humsaidia mchezaji kujenga mwili vizuri na kuimarisha afya na hata misuli ya mwanadamu.
tchoukball huchezwa na jinsi zote,wanaume na wanawake ni mchezo usiobagua jinsi ya mtu.
wote mnakaribishwa kujifunza mchezo huu na kujifunza ni bure kabisa,hakuna kulipia ila ada yako ni wewe kujituma katika kujifunza tchoukball,ada yako ni wewe kujituma katika kujifunza mchezo huu,ni bure kabisa na hakuna malipo .
Kwa maelezo zaidi wasiliana na kwa namba 0655519736 na kama ungependa kuona picha za mafunzo ya mchezo huu na video pia,PM namba yako kwangu na tutakutumia picha na hata video na kama utapenda tutakuunga ktk group ya watsapp ya Arusha Tchoukball kwa maelezo na mafunzo zaidi.
TCHOUKBALL.
 
Tupia kwanza hapa hizo picha ueleweke.

Inamaana gani mtu kuja inbox (PM) wakati uwezekano wa kutupia hapa upo?
 
Tupia kwanza hapa hizo picha ueleweke.

Inamaana gani mtu kuja inbox (PM) wakati uwezekano wa kutupia hapa upo?

natumia simu haina uwezo kutuma picha kwa mtandao wa jamiiforums ila unaweza kutazama pia picha kupitia page yetu ya fb ya Tanzania tchoukball.
Ila tutafanya mpango tuwaletee na picha kabisa ila kwa sasa hapa nilipo natumia simu.
 
Back
Top Bottom