Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Salaam wakuu, natumai nyote mpo salama
Ndugu zangu kijana wenu nimekuwa mtumiaji wa mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwamo Telegram, Instagram, Twitter na mingineyo.
Kama utakukubaliana na Mimi ukipita kwenye mitandao hii Kuna kiwango kikubwa Cha biashara ya ngono (umalaya) inayohusisha watu kutangaza kujiuza au madalali wanaojinasibu kuuza wengine kingono.
Miaka mitano nyuma biashara hii ilikuwa kwa kiwango cha chini lakini kwa sasa imezidi kuwa tishio. Ukipita kwenye comments za page za habari, viongozi au watu maarufu utakutana na watu wakijinasibu kuwa na hamu ya kufanya mapenzi huku wakiweka namba zao kusisitiza watafutwe ili watoe huduma.
Zaidi ya hayo, biashara hii ya ngono mtandaoni imepiga hatua za kuvunja kabisa maadili ya Watanzania kwa kutangaza biashara za ushoga na kusagana wazi wazi.
Nawaangushia zigo hili TCRA kwa sababu watu wanafanya biashara hizi wanaweka namba zao wazi kabisa mitandaoni.
Nachojiuliza hapa ni kwamba je Mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa Mitandao (TCRA) hawaoni haya?
Kama wanaona wanafanya jitihada gani kudhibiti biashara hizi hasa ukizingatia watu wanaweka mawasiliano yao na wao Wana Mamlaka ya kudhibiti.
TCRA msijifanye hamuoni, msichague vitu vya kudhibiti. Biashara hizi zinaathari kubwa sana kwa sababu mitandao kwa sasa inatumiwa na watoto, Vijana na wazee.
Tafadhali chukueni hatua.