TCRA fahamuni kuwa Watanzania ni waelewa kuliko mnavyodhani

TCRA fahamuni kuwa Watanzania ni waelewa kuliko mnavyodhani

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Jana jioni nilikuwa namsikiliza kipindi cha JAHAZI cha Clouds Radio.

Studioni alialikwa mkurugenzi wa TCRA ambaye alitoa fafanuzi mbalimbali kuhusu kuhakiki namba za simu na alielezea mwishoni kuhusu kupanda kwa gharama za mitandao.

Bahati mbaya sana vipindi vingi vya redioni ambavyo watangazaji wamegeuka kuwa ndiyo wachambuzi vimekuwa vya upande mmoja na kukosa ladha hasa pale watangazaji wanapoongelea masuala yanayoathiri jamii. Laiti wangelikuwa wanaruhusu wasikilizaji kushirikj mubashara ingeweka uwiano mzuri.

Kwenye issue ya kupanda kwa gharama za mitandao, mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano aliongea kuwa Tanzania gharama za huduma za mitandao hususan bando za internet zipo chini sana kulinganisha nchi za Afrika Mashariki na jumuiya ya SADC.

Watangazaji wa JAHAZI walijazia majibu ya mkurugenzi huku wakiwatupia lawama wamiliki wa simu mpanguso kuwa na matumizi yasiyo sahihi na kupakua apps ambazo zina opperate background.

Nilitamani kupata wasaa wa kumsaili mkurugenzi kuhusu hili la bei
  1. Je gharama za mitandao kuwa chini kunaendana na uwiano wa mzunguko wa fedha?
  2. Je kipato halisi cha Mtanzania wa kati na wa chini kinawiana vipi na vipato vya wananchi wa nchi hizo hasa tukichukulia GDP per...
  3. Kwa nini mara nyingi kauli za TCRA zinazotolewa na viongozi wake waandamizi na hata waziri zimeelemea kutetea ukandamizwaji wa watumiaji wa huduma huku zikiwatetea watoa huduma za mitandao?
  4. TCRA imewahi kufanya tafiti zozote kuhusu athari na changamoto wsnazokutana nazo watumiaji wa huduma za mitandao?
  5. Mkurugenzi anapoeleza ongezeko la matumizi ya bando, atuelekeze tunapata wapi hizo data ili tuverify kuoanisha na tunachopitia?
TCRA na Serikali ielewe kwamba, kupanda kwa bei ya vyakula hakushushi mahitaji ya chakula kwenye jamii bali wananchi wanaumia sana kugharimia mahitaji hayo.

Pia ifahamike kuwa, hali ya sasa kisayansi na kiteknolojia imepelekea ongezeko la mahitaji muhimu ya binadamu kutoka
Chakula
Mavazi
Malazi
  • Elimu
  • Mawasiliano
  • Usafiri
Uzi tayari
 
Wataongea blah blah zao ila mwisho wa siku kupanda kwa gharama kumetokana na mzigo wa makato na kodi wanaobebeshwa makampuni ya mawasiliano.

Ifahamike kuwa kodi yoyote kwa makampuni haya humuangukia mlaji wa mwisho ambaye ni sisi wateja wa hayo makampuni.

Hapo Burundi ukiwa na 10k yako (ambayo ni sawa na 7k ya tzsh) unajiunga unlimited bundle la internet la kasi ya juu kwa mwezi mzima!
 
Wataongea blah blah zao ila mwisho wa siku kupanda kwa gharama kumetokana na mzigo wa makato na kodi wanaobebeshwa makampuni ya mawasiliano...
Viongozi wetu wanadhani sisi ni TABULARASA
 
Wataongea blah blah zao ila mwisho wa siku kupanda kwa gharama kumetokana na mzigo wa makato na kodi wanaobebeshwa makampuni ya mawasiliano. Ifahamike kuwa kodi yoyote kwa makampuni haya humuangukia mlaji wa mwisho ambaye ni sisi wateja wa hayo makampuni.

Hapo Burundi ukiwa na 10k yako (ambayo ni sawa na 7k ya tzsh) unajiunga unlimited bundle la internet la kasi ya juu kwa mwezi mzima!
Kumbe ndio maana tuliambiwa tuhamie Burundi
 
Wataongea blah blah zao ila mwisho wa siku kupanda kwa gharama kumetokana na mzigo wa makato na kodi wanaobebeshwa makampuni ya mawasiliano.

Ifahamike kuwa kodi yoyote kwa makampuni haya humuangukia mlaji wa mwisho ambaye ni sisi wateja wa hayo makampuni.

Hapo Burundi ukiwa na 10k yako (ambayo ni sawa na 7k ya tzsh) unajiunga unlimited bundle la internet la kasi ya juu kwa mwezi mzima!
Hata hapa TZ hatushindwi kuwa na bando hizo kwa gharama hizo hizo. Ni uroho, tamaa, roho mbaya na kutaka kuwabana wananchi wasiwe na uhuru wa kupata habari kwa urahisi. Ni mahusiano yasiyo na maadili kati ya makampuni na watawala.

Hatuna mtetezi katika hili na kibaya zaidi wananchi hatuna umoja.
 
Na mimi leo asubuhi nimemsikia Msigwa( msemaji wa serikali.

Nikaelewa
Serikali ndio wameamua kuyabana makampuni yapandishe bei.
Lengo serikali ipate faida.

Kwamba hapo awali makampuni yalikuwa yanashusha bei, hadi serikali ikawa haipati faida nzuri.

Hapohapo anasema, wana mpango wakuangalia namna ya kupunguza gharama.

Hii ni aina nyingine ya Tozo.
 
Kupandisha gharama za mawasiliano siyo initiative ya makampuni husika, ni intererence ya serikali ili wakusanye tozo za kutosha kwenye hiyo sekta ya mawasiliano. Haijawahi kutokea kwenye biashara ya kiushindani kama ya mawasiliano makampuni yakawa na viwango vya data na bei zinazolandana.....​
 
Kupandisha galama za bando kwa wengne sio ttzo ttzo ni kutokuboresha bando iko juu na bado haina speed nzuri apo ndo ttzo linapoanzia
Lakin pia kutafta kodi na tozo kwa njia harari nazan serikal iko sawa kulko yule mungu mtu aliekua anaingua kwenye account zetu za bank na kuchukua pesa bira kibali wala ruhusa ya mwenye account

Lakin pia ifikie hatua tujue tu jmn sio lazima utumie internet na sizan km internet ni huduma ya muimu sana kwa binaadamu
Vtu vingne ni luxury unanunua tu sabu umependa mwenyewe

Km unatumia internet kufanya biashara bas ongeza na galama za bando kwenye bidhaa,

Vyombo vya habari haviwezi na wala havijawai kua mtetezi kwa mtanzania ata sku moja vyombo ving vya hbr vya Tz vinafanya biashara na makampuni makubwa ya simu ndo wazamin wao wakubwa na wamiliki weng wa vyombi vya habari ni Ccm
 
Jana jioni nilikuwa nasimiliza kipindi cha JAHAZI cha Clouds Radio.

Studioni alialikwa mkurugenzi wa TCRA ambaye alitoa fafanuzi mbalimbali kuhusu kuhakiki namba za simu na alielezea mwishoni kuhusu kupanda kwa gharama za mitandao.

Bahati mbaya sana vipindi vingi vya redioni ambavyo watangazaji wamegekua kuwa ndiyo wachambuzi vimekuwa vya upande mmoja na kukosa ladha hasa pale watangazaji wanapoongelea masuala yanayoathiri jamii. Laiti wangelikuwa wanaruhusu wasikilizaji kushirikj mubashara ingeweka uwiano mzuri.

Kwenye issue ya kupanda kwa gharama za mitandao, mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano aliongea kuwa Tanzania gharama za huduma za mitandao hususan bando za internet zipo chini sana kulinganisha nchi za Afrika Mashariki na jumuiya ya SADC.

Watangazaji wa JAHAZI walijazia majibu ya mkurugenzi huku wakiwatupia lawama wamiliki wa simu mpanguso kuwa na matumizi yasiyo sahihi na kupakua apps ambazo zina opperate background.

Nilitamani kupata wasaa wa kumsaili mkurugenzi kuhusu hili la bei
  1. Je gharama za mitandao kuwa chini kunaendana na uwiano wa mzunguko wa fedha?
  2. Je kipato halisi cha Mtanzania wa kati na wa chini kinawiana vipi na vipato vya wananchi wa nchi hizo hasa tukichukulia GDP per...
  3. Kwa nini mara nyingi kauli za TCRA zinazotolewa na viongozi wake waandamizi na hata waziri zimeelemea kutetea ukandamizwaji wa watumiaji wa huduma huku zikiwatetea watoa huduma za mitandao?
  4. TCRA imewahi kufanya tafiti zozote kuhusu athari na changamoto wsnazokutana nazo watumiaji wa huduma za mitandao?
  5. Mkurugenzi anapoeleza ongezeko la matumizi ya bando, atuelekeze tunapata wapi hizo data ili tuverify kuoanisha na tunachopitia?
TCRA na Serikali ielewe kwamba, kupanda kwa bei ya vyakula hakushushi mahitaji ya chakula kwenye jamii bali wananchi wanaumia sana kugharimia mahitaji hayo.

Pia ifahamike kuwa, hali ya sasa kisayansi na kiteknolojia imepelekea ongezeko la mahitaji muhimu ya binadamu kutoka
Chakula
Mavazi
Malazi
  • Elimu
  • Mawasiliano
  • Usafiri
Uzi tayari
Good observation.....
 
Nape ndio tatizo hiyo Sekta
Nape angekuwa tatizo angeshashughulikiwa na CCM pamoja na serikali.

Tatizo ni CCM inalipa fadhila kwa wanaochangia bajeti yao ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom