TCRA fahamuni kuwa Watanzania ni waelewa kuliko mnavyodhani

TCRA fahamuni kuwa Watanzania ni waelewa kuliko mnavyodhani

Wataongea blah blah zao ila mwisho wa siku kupanda kwa gharama kumetokana na mzigo wa makato na kodi wanaobebeshwa makampuni ya mawasiliano.

Ifahamike kuwa kodi yoyote kwa makampuni haya humuangukia mlaji wa mwisho ambaye ni sisi wateja wa hayo makampuni.

Hapo Burundi ukiwa na 10k yako (ambayo ni sawa na 7k ya tzsh) unajiunga unlimited bundle la internet la kasi ya juu kwa mwezi mzima!
Upo sahihi
 
Apps ya facebook ilianza ikiwa na mb 20 mwanzo ila sasa app ya facebook inafika mb 400.
Hapo ujatumia na ukitumia inaongezeka kufika 1gb na kitu.

Update ya simu inataka 2gb na kuendelea.

Leo hii internet ni anasa.kuna siku nilieleza EFD mashine wakati rekodi zako zipo TRA lakini unalazimishwa kuja na makaratasi ya risiti.
 
Jana jioni nilikuwa namsikiliza kipindi cha JAHAZI cha Clouds Radio.

Studioni alialikwa mkurugenzi wa TCRA ambaye alitoa fafanuzi mbalimbali kuhusu kuhakiki namba za simu na alielezea mwishoni kuhusu kupanda kwa gharama za mitandao.

Bahati mbaya sana vipindi vingi vya redioni ambavyo watangazaji wamegeuka kuwa ndiyo wachambuzi vimekuwa vya upande mmoja na kukosa ladha hasa pale watangazaji wanapoongelea masuala yanayoathiri jamii. Laiti wangelikuwa wanaruhusu wasikilizaji kushirikj mubashara ingeweka uwiano mzuri.

Kwenye issue ya kupanda kwa gharama za mitandao, mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano aliongea kuwa Tanzania gharama za huduma za mitandao hususan bando za internet zipo chini sana kulinganisha nchi za Afrika Mashariki na jumuiya ya SADC.

Watangazaji wa JAHAZI walijazia majibu ya mkurugenzi huku wakiwatupia lawama wamiliki wa simu mpanguso kuwa na matumizi yasiyo sahihi na kupakua apps ambazo zina opperate background.

Nilitamani kupata wasaa wa kumsaili mkurugenzi kuhusu hili la bei
  1. Je gharama za mitandao kuwa chini kunaendana na uwiano wa mzunguko wa fedha?
  2. Je kipato halisi cha Mtanzania wa kati na wa chini kinawiana vipi na vipato vya wananchi wa nchi hizo hasa tukichukulia GDP per...
  3. Kwa nini mara nyingi kauli za TCRA zinazotolewa na viongozi wake waandamizi na hata waziri zimeelemea kutetea ukandamizwaji wa watumiaji wa huduma huku zikiwatetea watoa huduma za mitandao?
  4. TCRA imewahi kufanya tafiti zozote kuhusu athari na changamoto wsnazokutana nazo watumiaji wa huduma za mitandao?
  5. Mkurugenzi anapoeleza ongezeko la matumizi ya bando, atuelekeze tunapata wapi hizo data ili tuverify kuoanisha na tunachopitia?
TCRA na Serikali ielewe kwamba, kupanda kwa bei ya vyakula hakushushi mahitaji ya chakula kwenye jamii bali wananchi wanaumia sana kugharimia mahitaji hayo.

Pia ifahamike kuwa, hali ya sasa kisayansi na kiteknolojia imepelekea ongezeko la mahitaji muhimu ya binadamu kutoka
Chakula
Mavazi
Malazi
  • Elimu
  • Mawasiliano
  • Usafiri
Uzi tayari
Waandishi wanaogopa kuhoji in deep wakihofu kufukuzwa kazi!
 
Nepi aliwahi kusema wazazi wake walijitoa kupigania nchi hii wakafa bila kumiliki kitu chochote lakini yeye hawezi kukubali aende mtupu chochote kitakachotokezea mbele yake ataupiga mwingi. kwa hiyo TCRA ni matokeo ya kuupiga mwingi.
 
Hawa wanahabari ni low brain ni wale unga unga hakuna one na two. Unadhani wanauwezo wa kuhoji jamb9 lolote? Labda bahasha
 
Back
Top Bottom