TCRA fungia vipindi vya Uhondo na Sasambua

TCRA fungia vipindi vya Uhondo na Sasambua

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2008
Posts
1,933
Reaction score
988
Kuna vipindi vinarushwa na FM radio zinazorusha matangazo yao kutokea jiji la Dar es salaam.
Vipindi hivi ni vile Uhondo na Sasambua.

Ukweli ni kuwa, japo vimeendelea kurushwa kwa muda mrefu, kimaadili vipindi hivi havijengi jamii bali vinaiharibu kidogo kidogo. Wakati kipindi cha Uhondo kinaongezea lugha ya kunyanyapaa mwanajamii kile cha Sasambua, kinapandikiza chuki na kuifundisha jamii hasa watoto namna ya kuwa mtukanaji.

Watangazaji wote wa vipindi hivyo wanachekelea sana mambo ya aibu yanayotamkwa na wageni wa vipindi vyao.

TCRA, inusuru jamii ya Kitanzania.
 
wewe mwenyewe unapata wapi muda wa kusikiliza upuuzi kama huo?
 
Kwa sababu hiyo, basi na hii miziki karibia yote ya kizazi kipya ifungiwe/ifutwe. Maana nayo inaharibu jamii 'kidogp-kidogo'
 
Naomba uweke kwenye list miziki karibia yote ya WCB, akiongozwa na baba lao
 
For sure nyimbo nyingi za bongoflava sasa hivi hazifai kusikilizwa na jamii.

Badala ya kuimba mapenzi wao wanaimba tendo la ndoa/ ngono.

Na watoto wetu wakizisikiliza wanaanza kutuimbia kama vile ni nzuri

Katika jamii iliyostaarabika hizi nyimbo hazifai.
Kwa sababu hiyo, basi na hii miziki karibia yote ya kizazi kipya ifungiwe/ifutwe. Maana nayo inaharibu jamii 'kidogp-kidogo'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
For sure nyimbo nyingi za bongoflava sasa hivi hazifai kusikilizwa na jamii.

Badala ya kuimba mapenzi wao wanaimba tendo la ndoa/ ngono.

Na watoto wetu wakizisikiliza wanaanza kutuimbia kama vile ni nzuri

Katika jamii iliyostaarabika hizi nyimbo hazifai.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ile ya kugusanisha hasi na chanya....nyama kwa nyama yule maua sama kaimba porno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom