Mkoba wa Mama
JF-Expert Member
- May 5, 2021
- 280
- 173
Hii imenitokea leo, nilienda kubadili laini ya Vodacom ili nipate laini ya 5G, wakala akaniambia niweke finger print, niliweka mara mbili baada ya kusema mara ya kwanza nilikosea. Baada ya kumaliza zoezi hilo na kuondoka pale, nilipokea ujumbe mfupi kutoka Airtel kuwa nimesajili laini mpya ya Airtel kwa kutumia NIDA yangu, wakati mimi sikusajili laini ya Airtel wala nyingine yoyote zaidi ya kuomba kubadilishiwa laini yangu ya Vodacom kuwa ya 5G.
Ilibidi niwapigie Airtel, kwa namna walivyonielezea nikagundua yule wakala ndiye alitumia namba yangu ya NIDA kusajili hiyo laini ya Airtel.
Tuwe makini sana na hawa mawakala, lakini pia mamlaka husika ziangalie hii njia ya kusajili laini maana kwa sasa imekua ni holela sana, pia TCRA iwe inafuatilia kwa karibu sana na kufanya uchunguzi wa kutosha pale mtu anaporipoti namba iliyohusika na utapeli, maana kama mawakala wanatumia njia hii bila mmiliki wa NIDA kufahamu, suala hili litawaingiza watu wengi (wenye NIDA) kwenye hatia wakati wahusika ni wengine (mawakala) wakiachwa na kuendelea na uhalifu.