TCRA imezindua tena kampeni ya elimu kwa umma iitwayo "Futa delete kabisa"

TCRA imezindua tena kampeni ya elimu kwa umma iitwayo "Futa delete kabisa"

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw. Rolf Kibaja, ametoa wito kwa umma kutumia huduma za mawasiliano kwa njia sahihi na salama.

TCRA imezindua tena kampeni ya elimu kwa umma iitwayo “FUTA DELETE KABISA”, ikilenga kuendelea kusisitiza matumizi bora ya huduma za mawasiliano na kuwakumbusha watumiaji wajibu wao wa kusambaza taarifa sahihi na zenye uthibitisho, pamoja na kufuta na kuepuka kusambaza ujumbe au taarifa zenye kuchochea upotoshaji, uzushi, chuki, na uvunjifu wa amani.

Bw. Kibaja aliyasema hayo , Ijumaa Agosti 8, 2025, katika kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane)

 
Back
Top Bottom