TCRA ina 'task force' ya kuwashughulikia wenye televisheni za online ambazo hazijasajiliwa

TCRA ina 'task force' ya kuwashughulikia wenye televisheni za online ambazo hazijasajiliwa

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Engineer Kisaka ameyasema hayo leo Septemba 16, 2022 wakati wa Warsha ya Kuhamasisha Uandaaji, na Uzalishaji wa Maudhui ya Ndani iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambapo Waziri wa Habari na Mawasiliano.

"…lazima tumsikilize kila mmoja anasemaje. Muafaka uliofikiwa ni kuwa watu wafanye kazi zao mtandaoni. Lakini anayefanya kazi ya kiuanahabari, ya mawasiliano. Yule ambaye Waziri akija anaweka ka-mike kake hapa, gari likianguka kule Kondoa anataka atoe taarifa, anafanya kazi zinazofanana na media – hawa ndiyo wapewe leseni."

"Tumekusanya orodha ndefu sana ya unlicensed…na hamjui, wananyakuliwa mmoja baada ya mwingine. Hapa ninavyosema nina listi ndefu sana. Na kuna watu wanatoa shutuma, wanatukana watu; kuna zile za ngono nadhani pia mnaziona."

"Kwahiyo hilo linafanyiwa kazi kikamilifu. Kuna special task force inalifanyia hilo kazi. Sema hii inahitaji muda, siyo kama ile unajua yupo pale unaenda kumnyakua.Kwahiyo unaenda naye taratibu mpaka unapompata unakuwa umetumia resources na muda mwingi."

Pia amesema Suala hili halitangazwi lakini itafika kipindi matokeo yataonekana.
 
Back
Top Bottom