TCRA, inakuwaje magazeti ya Uhuru na Jamvi la Habari hayajafungiwa kwa kuripoti habari sawa na Clouds Media?

TCRA, inakuwaje magazeti ya Uhuru na Jamvi la Habari hayajafungiwa kwa kuripoti habari sawa na Clouds Media?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
Hapa kuna tofauti gani au nayo ni sehemu ya kuendeleza udhalimu na kutishia vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu kutotangaza habari za upinzani.

IMG_20200827_200203.jpg


IMG_20200827_172959.jpg
Screenshot_20200827-205906.png
 
Bado jf kufungiwa.

Tutaona mengi ktk uchaguzi mkuu mwaka huu.
 
Hapa kuna tofauti gani au nayo ni sehemu ya kuendeleza udharimu na kutishia vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu kutotangaza habari za upinzaniView attachment 1549974View attachment 1549975
Jielimishe.

TCRA haisimamii Magazeti wala Majarida. Magazeti na Majarida yanasimamiwa na Idara ya Habari Maelezo ambayo ipo chini ya Wizara ya Habari. Idara hii ndiko hayo magazeti yanapata usajili na kusimamiwa. Hata wewe kama unahitaji kuanzisha gazeti utaenda huko.

TCRA inasimamia vyombo vya Utangazaji, Simu,Posta,na Mawasiliano yote ya Kielektroniki zikiwemo redio call,mawasiliano ya ndege, kuthibitisha vyombo vipya vya mawasiliano, mambo ya vipeto kv DHL, mambo ya mkongo nk nk wakiwemo online media, coded number kv *150*01# nk nk...

Kwa hiyo malalamiko yako haya yawasilishe Idara ya Habari Maelezo.

Ni muhimu tujenge utamaduni wa kujifunza juu ya vitu vyetu ndugu watanzania ili tuelewe mifumo yetu kiukamilifu.

Wasalaam!.

N'yadikwa
 
Back
Top Bottom