Ni wito kwa TCRA ishirikiane na Shirika la Mawasiliano la Kenya kuwasaka matapeli hawa wa mitandaoni. Huu utapeli wa mtandaoni umevuka mpaka kutoka kuwa wa Kitaifa sasa ni utapeli kimataifa. Namba za simu zifuatavyo ni baadhi ya zinazotumiwa na matapeli, +254794812691 (Alex Kairi), +254102269805 (Rusi Sigel) na +254102143329. Katika utapeli wao wanatumia jina UNICEF Foundation Funds. Tahathari kwa wote juu ya utapeli huu. Mods tafadhalini huu uzi usichanganywe na zingine ili ibaki wito kwa TCRA ishirikiane na Shirika la Mawasiliano la Kenya kuwasaka matapeli wa mtandaoni. Nawasilisha.