Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Kazi moja kubwa ya TCRA toka wakiwa kitengo cha kudhibiti masafa ya kurusha mawimbi ya redio wakiwa Posta na Simu(TP &TC), ilikuwa kuangalia ni nani anarusha mawimbi yake katika masafa yepi.
Sasa hivi tuna TCRA ambao siyo siri wana mitambo mikubwa na makini zaidi lakini wasomi hapo na mainjinia ni wengi zaidi.
Majuzi nikiwa nasikiliza redio ya gari yangu nikafungulia masafa ya 92.5 MHz.
Nilikuwa nasikiliza zilipendwa, mara baada ya dakika fulani nasikia mawahidha ya kiislamu, mara mtangazo mengine.
Nikajaribu ku fine tune lakini tatizo likawa pale pale.
Siwalaumu wenye redio, nailaumu TCRA, inaelekea wanaanza kushindwa kazi ya kiuhandisi ya ku monitor matumizi ya masafa.
Aidha wametoa leseni za masafa karibu karibu sana yaani wameuza 92.3, 92.4 na 92.5 hivyo muingiliano au uzembe tu wa ku monitor matumizi ya masafa.
Kwa kweli inakera wakati ukisikiliza kipindi pendwa, halafu kinaingiliwa na masfa mengine.
Wajuvi wa sheria ya mawasiliano mtujuze na mpo mnaoifahamu hiyo sheria, tunaweza vipi kuishitaki TCRA kwa huduma mbovu wanayotoa kwa umma.
Kiukweli wao TCRA wanakuwa wakali katika ku monitor content ya matangazo na kupiga fine kubwa kubwa.
Wasikilizaji je tuchukue hatua zipi kulishitaki hili shirika kwa uzembe wa wazi?