TCRA kuondoa vocha za kukwangua kuanzia Januari 2027.

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2009
Posts
19,009
Reaction score
22,509

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza mpango wa kuondoa matumizi ya kadi za kukwangua za muda wa maongezi ili kuongeza matumizi ya njia za kidijitali.

TCRA imesema mpango huo utachangia kupunguza uzalishaji, usambazaji na utupaji wa kadi za kukwangua za muda wa maongezi pamoja na athari zake kwa mazingira, huku ukiunga mkono maendeleo ya sekta ya mawasiliano yenye ufanisi na inayotumia teknolojia za kidijitali.

Aidha, imeongeza kuwa zoezi la majaribio ya kusitisha matumizi ya kadi hizo litaanza Januari 1, 2027 likitanguliwa na shughuli za uhamasishaji kwa umma zilizoanza Oktoba 1, 2026.

TCRA imesema zoezi la majaribio litahusisha Mkoa wa Dar es Salaam, Dodoma (Jiji la Dodoma, Chamwino, Kondoa Mjini na Kongwa), Arusha (Jiji la Arusha, Wilaya ya Arusha, Meru na Karatu), Mwanza (Nyamagana, Ilemela na Misungwi) na Mbeya (Jiji la Mbeya, Wilaya ya Mbeya na Mbarali).

Chanzo:-
TCRA kuondoa vocha za kukwangua kuanzia Januari 2027 · SwahiliTimes TCRA kuondoa vocha za kukwangua kuanzia Januari 2027 · SwahiliTimes
 
Huko vijijini itakuwa balaa na fursa kama vocha ya kukwangua kuna watu hawawezi kuingiza na kujiunga kifurushi
Ngoja tusubiri tuone!
 
Mbona hatujawahi kuwaomba waziondoe? Kuna watu tuna vimeo vya songesha na nipige tafu. Tutakimbilia wapi?
 
Safi sana

N vyema wanaanza na mijini mana vijijini huko ndani ndani ingekuwa changamoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…