Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Vitendo vilivyoripotiwa vya ulaghai kwenye mitandao ya simu vimepungua kwa asilimia 28 kati ya Juni na Septemba mwaka huu, kutokana na hatua kali za serikali na kampeni za kuongeza uelewa wa watumiaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt Jabiri Bakari, alifichua katika Ripoti ya hivi karibuni ya Takwimu za Utendaji wa Sekta kuwa majaribio ya ulaghai yalipungua kutoka 22,267 Juni 2024 hadi 16,069 mwishoni mwa Septemba, pia alisema ushirikiano mkubwa kati ya wadau muhimu, wakiwemo watoa huduma za simu pia ni jambo muhimu katika mafanikio hayo.
Katika azma mpya ya serikali ya kupambana zaidi na vitendo vya uhalifu, hivi karibuni wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia ya habari na mambo ya ndani iliitisha mkutano wa ngazi ya juu wa wadau ili kushughulikia utapeli wa mitandao na usalama wa mitandao, washiriki wakiwaa wenye leseni za mitandao ya simu za mkononi na wadau wengine wa usalama mtandaoni.