TCRA mpo???TIGO wameoza!

munisijo

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
1,126
Reaction score
942
Inaonekana baada ya TIGO kuzawadiwa nafasi ya kwanza kwa kutoa huduma mbovu na kutowasikiliza wateja, sasa wameamua kudhibitisha hilo kwa vitendo.
Kwa wiki sasa TIGO wamekua na matatizo makuu ya mtandao lakini badala ya kutoa taarifa kwa wateja tujue cha kufanya, wao wameendelea kukenua meno maofisini mwao hadi sasa.
Kikubwa wanachojua wao ni kufanya promotion,matangazo na kutuma SMS lukuki kila kukicha tena bila hiyari ya mteja ili waweze kuwaingiza watu wengi zaidi kwenye uozo wao, ukiuliza salio kabla hawajakujibu kwanza, lazima wakuwekee matangazo lukuki...hivyo hivyo ukipiga, ukimkosa uliyempigia ama unayempigia akiwa anatumia simu...sijawahi kuona uozo kama huu!
Haya sasa, uwe na shida kuu na unahitaji kuongea nao moja kwa moja, hapo ndipo utakapo choka, watakuzungua wee na mwisho wa siku et wanakuambia uache ujumbe kwenye mtandao kisha watakupigia watakapojisikia. Nasikitika kusema leo na shida/kero zangu ni zaidi ya mara 10 nimejaribu kuwapata bila mafanikio na simu yao nimeingoja hadi nimechoka! Ni wapi ambapo mtoa huduma ana nguvu kuliko mteja...???!!!Sijawahi kuona...
Sijajua huwa wanawadanganya nini TCRA wasiwachukulie hatua hadi sasa.Kwa ujumla TIGO kihuduma, wameoza!
 
ndugu huu mtandao ni tatizo sana kero iliyo kithri
 
Tena kuna kipindi nikawa naweka weka salio kwenye akaunti yao kwenye lain yangu ila baada ya kubaini uozo walionao hakika niliikangua yote na hata hivyo nina mpango wa kuifutilia mbali mtandao huu wa kijinga ndani ya Taifa letu!
 
wote nyie mnalipwa na makampuni ya mafisadi nini?.povu loe la nini? mbona sie tunapiga tu kwa kwenda mbele na internet full day.
 
Hii kitu inaniuzi sana, ukipiga simu kama haipatikani wanakuwekea matangazo weee halafu ndiyo baadaye wanakwambia simu unayopiga haipatikani au inatumika. Mimi situmii mtandao wa Tigo, lakini nakutana na hali hii wakati napiga namba za tigo, na naamini watu wengi watakuwa wanakutana na hali hii ikiwemo maafisa wa TCRA na viongozi wakuu wa serikali, lakini kwa sababu system ya utawala wa nchi imeoza hakuna wa kuchukua hatua.
Nawashauri tupieni kwenye kapu hizo laini za tigo wakiona wateja wanaisha lazima watashtuka vingenevyo watakuwa kama Tritel.
 

Ebu nifafanulieni Mtandao Mzuri Ukoje wana Jamiii.
 
Watakua wametumwa na kampuni ya Mafisadi tena pesa za wananchi. tiGo full shangwe hakuna mambo ya Kibwege ya kikuda ya Kulia watu pesa kwenye promotion. eti ukijiunga cheka ata saa 23:55 siku hyohyo ikifika saa 24:00 eti masaa 24 yameisha( huu ni mtandao wa mafisadi wanaumiliki) lakn Tigo Ukijiunga extreme saa 12:00 itaisha baada ya masaa 24 yaani kesho 12:01. Mnaibiwa lkn bado tu
 
Ata Mitandao mnayoiita Mizuri Ukipiga simu unajbiwa not reachable wakati ipo hewani. Nyie mmetumwa wakuda
 
Hakuna Mtandao usio na Hizi tabia ulizo andika hapo juu hapa TZA, Mkuda wewe unakulupuka Kuconclude mambo bila fact
 
nimeuliza salio....wakaniuliza kama ninahitaji hotuba ya obama bure...nilivyotuma ndio wakaniunga na caller tunes....balaa tupu
 
Rahisi unahama mtandao maana ipo mingi sasa nenda Voda,Airtel,Zantel
 
Ebu nifafanulieni Mtandao Mzuri Ukoje wana Jamiii.

Mtandao mzuri ni ule unaopatikana 24/7 na kama utakosekana hata kwa nusu saa basi ukirudi wateja wanajulishwa kuwa kulikua na shida ama kama wanajua kama maybe kesho saa tatu kutakuwa na shida then wateja wanakuwa informed in advance.Pia mtandao mzuri ni ule ambao atleast ukiwa safarini usitembeee zaidi ya saa nzima bila kukutana na network coverage, mtandao mzuri ni ule unapopiga customer care unapata majibu ya kuridhisha na kama sio kujitosha ambayo yanaweza kumtia moyo customer
 
Hivi bado kuna watu wanatumia togo?
 
Vodacom: hivi ni kwa nini lakini?
Siku hizi hawa Jamaa wamekuwa na mtindo wa kutujazia wateja Inbox zetu kwa Meseji juu ya Products/Services zao mpya (ambazo hata hivyo huwa hazidumu).. Hii ni Tabia ya Tigo, Voda wameamua kuiga?
Siku hizi Vodacom wamekuwa wakianzisha Products/Services ambazo huwa hazikai sana, wanaziondoa.
Siku hizi Menu ya Vodacom inabadilika badilika kila mara bila maboresho ya msingi (wakati mwingine haipatikani)
Je kitengo cha Masoko cha hii Kampuni hakifanyi Utafiti na kujiridhisha kabla ya kuruhusu bidhaa iingie sokoni?
Yaani ni kama vile wako desperate na kitu fulani hivyo wanakurupuka kufanya maamuzi ili wajiokoe..
Hii Bima ya Vodacom faraja ni kama kuwaambia watu kufeni ili tuwalipe ndugu zenu, kwa nini hawakuanzisha Bima ya Afya ili inufaishe watanzania wenye mahitaji ya huduma za Afya (na kuwaepusha na vifo) kuliko kusubiri tufe ili watoe kifuta machozi kwa ndugu zetu?
Kwa upande wa M-Pesa pia kuna matatizo ya mara kwa mara, message delay, transaction cancellation n.k

Binafsi nauchukulia huu Mtandao kama 'wenye afadhali' kulinganisha na mitandao mingine, lakini hizi kero za mara kwa mara zinakatisha tamaa sasa.

Rene Meza, hebu rekebisha hizi kero Bana.

Mapendo
TANMO​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…