munisijo
JF-Expert Member
- Apr 10, 2012
- 1,126
- 942
Inaonekana baada ya TIGO kuzawadiwa nafasi ya kwanza kwa kutoa huduma mbovu na kutowasikiliza wateja, sasa wameamua kudhibitisha hilo kwa vitendo.
Kwa wiki sasa TIGO wamekua na matatizo makuu ya mtandao lakini badala ya kutoa taarifa kwa wateja tujue cha kufanya, wao wameendelea kukenua meno maofisini mwao hadi sasa.
Kikubwa wanachojua wao ni kufanya promotion,matangazo na kutuma SMS lukuki kila kukicha tena bila hiyari ya mteja ili waweze kuwaingiza watu wengi zaidi kwenye uozo wao, ukiuliza salio kabla hawajakujibu kwanza, lazima wakuwekee matangazo lukuki...hivyo hivyo ukipiga, ukimkosa uliyempigia ama unayempigia akiwa anatumia simu...sijawahi kuona uozo kama huu!
Haya sasa, uwe na shida kuu na unahitaji kuongea nao moja kwa moja, hapo ndipo utakapo choka, watakuzungua wee na mwisho wa siku et wanakuambia uache ujumbe kwenye mtandao kisha watakupigia watakapojisikia. Nasikitika kusema leo na shida/kero zangu ni zaidi ya mara 10 nimejaribu kuwapata bila mafanikio na simu yao nimeingoja hadi nimechoka! Ni wapi ambapo mtoa huduma ana nguvu kuliko mteja...???!!!Sijawahi kuona...
Sijajua huwa wanawadanganya nini TCRA wasiwachukulie hatua hadi sasa.Kwa ujumla TIGO kihuduma, wameoza!