TCRA: Sasa vifurushi vimerudi kama awali

TCRA: Sasa vifurushi vimerudi kama awali

MPUNGA MMOJA

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2015
Posts
304
Reaction score
401
“Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kuwajulisha kwamba sasa vifurushi vya mawasiliano ya simu vimerudi kama awali, endapo kuna Mwananchi bado anapata changamoto ya huduma hii tuandikie TCRA

====

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetaarifu kuwa vifushi vya mawasiliano vimerudi kama awali. Kama kuna mwananchi anachangamoto anaweza kuwaandikia kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii

Vifurushi vilipanda bei Aprili 1, ambapo wananchi walilalamikia bei mpya kwa kuwa ziliongezeka kwa zaidi ya 100% na TCRA wakaamuru bei zirudi kama awali
 
Ngoja nihakikishe, halafu ntarudi na update.

Nchi yetu ilipofikia sasa hivi, ukiona taarifa hata kutoka kwa Rais au Waziri usiamini kabisa, lazima uhakikishe ili ujiridhishe kwanza.

updates

Tigo & Airtel hawajarudisha bado, Bundle zipo vile vile. Tigo Tshs 1000/= unapata MB 300. Baada ya kujiridhisha nathubutu kusema TCRA ni waongo.!!!
 
IMG_20210430_035654.jpg

Kichwa Cha habari kilipaswa kuwa..TCRA yasalimu amri kwa makampuni ya simu.
 
Well, tigo walikuwa wananipa 900 min, 9GB na SMS 500 kwa mwezi 20,000, wakapunguza wakawa wananipa dakika hizo hizo na SMS pia ila GB wakawa wananipa 4 kwa bei hiyo hiyo 20,000 kwa mwezi.

Ila tangu juzi naona wamerudisha na kama wameongeza bundle kidogo, nimejiunga jana nimepata 1500 min, SMS 500 na GB 10 kwa 20,000/month.

Therefore inategemea line na line may be...!

Screenshot_20210430-042452.png
 
Labda kwa upande ndiyo wamerudishiwa vifurushi ila kwa wanyonge hakuna kitu!

Ova
 
Well, tigo walikuwa wananipa 900 min, 9GB na SMS 500 kwa mwezi 20,000, wakapunguza wakawa wananipa dakika hizo hizo na SMS pia ila GB wakawa wananipa 4 kwa bei hiyo hiyo 20,000 kwa mwezi.

Ila tangu juzi naona wamerudisha na kama wameongeza bundle kidogo, nimejiunga jana nimepata 1500 min, SMS 500 na GB 10 kwa 20,000/month.

Therefore inategemea line na line may be...!

View attachment 1768392
Tatizo jingine kwa hawa tigo ni huo upuuzi wao wa LONGA NAE
 
Back
Top Bottom