TCRA simamieni namba za simu zilizosajiliwa zisipate usajili mpya

TCRA simamieni namba za simu zilizosajiliwa zisipate usajili mpya

Mtu anafumgwa gerezani mwaka akitoka hana chake,
Ki ukweli hii ki usalama ni hatari sana
 
Hao Airtel nadhani mwezi tu wanaigawa namba. Mie nilishangaa sana line ipo kwenye simu, double line sema yenyewe sikuwa naitumia. Na niliiwekea muda wa maongezi kama buku 5, huwezi amini namba waliigawa. Nawauliza ohh hukuwa unaitumia. Haya rudisheni hela yangu wanambwela tu.
C.A.G afanye uhakiki wa hizi fedha zinazobakia huko
 
Salam kwenu.

Naona sasa imekuwa kero sana kwa makampuni ya simu kuamua kuzifanyia usajili upya namba simu kwa kigezo hazijatumika kati ya miezi 3 hadi 6.

Leo nimemtafuta mtu kwa namba ta tigo ambayo tulikuwa tukiwasiliana kwa muda mrefu isipokuwa siku za karibuni. Naastaajabu anapokea mtu tofauti.

Kuna siku nimerekebisha simu iliyokufa, niliacha line humo naashangaa haifanyi kazi, naambiwa imepewa usaji kwa mtu mwingine.

Leo pia kuna jamaa analalamika ameenda benk kukopa, anaambiwa namba yake inaonekana alishakopa akatelekeza deni.

Labda TCRA watusadie, ulazima ni upi kuruhusu usajili upya kwa namba ambazo hazitumiki.

Hizi ni identity za watu na ambazo zinaacha alama, tunazungumzua kanzi data binafsi. Sheria yetu inasemaje kuhusu taarifa binafsi.

Fikiria namba yako leo ghafla imetumika na wale jamaa zetu tuma kwenye namba hii.

Soma Pia: TCRA: Utapeli wa "Tuma kwa Namba Hii" umepungua sana nchini


Vodacom Tanzania , Tigo, airtel.

Nadhani mnaweza kufanya kitu, kama namba hazitumiki ni heri mpate consent ya mtu ama mziweke inactive hadi hapo anapoweza kufika katika ofisi zenu na kurudisha tena huduma. Wengine huacha kutumia namba kwa muda kwa sababu tofauti tu.

Nina rafiki yangu alienda kusoma Nje ila kwa kuwa namba yake alisajili kwa kitambulisho cha Taifa hakupata hiyo changamoto.
Hebu tujiridhishe kwanza kama hizo namba wanazopewa watu wengine zilisajiliwa kwa kitambulisho cha TAIFA...
 
Nina rafiki yangu alienda kusoma Nje ila kwa kuwa namba yake alisajili kwa kitambulisho cha Taifa hakupata hiyo changamoto.
Hebu tujiridhishe kwanza kama hizo namba wanazopewa watu wengine zilisajiliwa kwa kitambulisho cha TAIFA...
Mimi zangu zote voda na airtrl nimezisajili na NI. Hapa bila kujali, hiyo namba umeisajili vipi ikiisha kutumika kwa mtu mmoja ibakie tu.
 
Back
Top Bottom