TCRA tusaidieni na haya matusi tunayotukanwa na matapeli

Kinengunengu

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2021
Posts
1,716
Reaction score
4,375
Leo nimepigiwa simu na namba 0653608556 akijifanya Mfanyakazi wa Tigo pesa na akasema akaunti yangu ya tigo pesa imefungiwa.

Jamaa akaanza nisomesha na akauliza simu yako ni smartphone au kiswaswadu. Nikasema kiswaswadu, akaniambia nibonyeze namba *37# sikubonyeza na yeye akajua kwamba sikubonyeza na simu yangu ni smartphone. Kilichofuata ni matusi mazito kwangu.

Kero hii imekuwa ni ya kujirudia, binafsi ni mara ya tatu au nne kunipigia na baada ya kuwashtukia wanatukana.

TCRA tusaidieni kuondoa hizi kero. Yaani jamaa anataka kukutapeli na ukishtuka anakutukana. Hii sio sawa. Tusaidieni lasivyo kuna siku tutachukua sheria mkononi kwa watu kama hawa.
 
Sasa unafikiri hao TCRA hawakutani na zahma kama hizo?

Hao unamalizana nao kihuni tu

Mi alinipigia juzi kajidai mtoa huduma akiuliza kutaka kujua changamoto za wateja

Nikamuambia changamoto kubwa ni matapeli wanaopiga simu kutumia namba binafsi na wakijidai custumer care wakati nyie mlishatupa muongozo kuwa mtawasiliana nasisi kupitia namba 100

Nikastukia mtu kakata simu
 
Kwa namna Tanzania yetu ilivyo mbovu kwenye kufuatilia,watu kama hao ni wa kuwapuuza tu

Mie kuna siku asubuhi nimeamka nikakuta namba ngeni imenitumia ujumbe wa pongezi kwamba nimejishindia kiasi cha 6M tatu mzuka....nikajikuta nacheka manake tatu mzuka yenyewe siijui

Sijakaa sawa simu ikaita wakaniambia nimejishindia tatu mzuka 6M kwa hiyo ili kupata hicho kiasi natakiwa niwatumie kiasi fulani

Nikawapa jibu jepesi tu kwamba sihitaji hizo 6M nikakata simu

Uzuri hawakujafanikiwa walichotaka
Pole mkuu
 
Hawa sisi wenyewe tunawa entertain

Alipopiga na ukiona ni miyeyusho

We ungempotezea tu au unamuweka hewani,Huna haja ya kumjibu

Ova
 
Screenshot_20220720-210932_Messages.jpg

Siku hizi huo ndo mwendo tu. Sipotezi mida!
 
Leo nimepigiwa simu na namba 0653608556 akijifanya Mfanyakazi wa Tigo pesa na akasema akaunti yangu ya tigo pesa imefungiwa.

Jamaa akaanza nisomesha na akauliza simu yako ni smartphone au kiswaswadu. Nikasema kiswaswadu, akaniambia nibonyeze namba *37# sikubonyeza na yeye akajua kwamba sikubonyeza na simu yangu ni smartphone. Kilichofuata ni matusi mazito kwangu.

Kero hii imekuwa ni ya kujirudia, binafsi ni mara ya tatu au nne kunipigia na baada ya kuwashtukia wanatukana.

TCRA tusaidieni kuondoa hizi kero. Yaani jamaa anataka kukutapeli na ukishtuka anakutukana. Hii sio sawa. Tusaidieni lasivyo kuna siku tutachukua sheria mkononi kwa watu kama hawa.
Hao ni wao TCRA wanatapeli watu, mbona walidukua mawasiliano ya Nape, kinana, makamba nk.
Ukiripoti hakuna hatua yoyote wanachukua.
 
Sasa unafikiri hao TCRA hawakutani na zahma kama hizo?

Hao unamalizana nao kihuni tu

Mi alinipigia juzi kajidai mtoa huduma akiuliza kutaka kujua changamoto za wateja

Nikamuambia changamoto kubwa ni matapeli wanaopiga simu kutumia namba binafsi na wakijidai custumer care wakati nyie mlishatupa muongozo kuwa mtawasiliana nasisi kupitia namba 100

Nikastukia mtu kakata simu
Nilipigiwa na mmoja akijifanya ni CC airtel.. ALipotaja jina tu kwamba anaitwa Nasibu, nikamwambia..NASIBU, ACHA BASI, UTAPELI WA HIVYO WA KIZAMANI.. CASTOMER CARE HAWAPIGI SIMU KWA NAMBA HIYO.. Alitukana matusi ya nguoni. Nikamwambia acha ushamba wa kutukana matusi ya zamani, tukana mapya..!! Akakata simu
 
Kwa namna hiyo tujue bado mfumo wetu wa kuwatambua Scammers ni mdogo au hauna nguvu za kutosha. Ni maoni yangu mwananchi ambaye nilitapeliwa kiasi cha pesa ya mboga japo iliniuma.
 
Tanzania hakuna ma IT tunasema siku zote hii kitu wapumbavu wanabisha ...pia hao wahuni wanao fanya haya mambo ni makada wa ccm na wengine ni watumishi wa makampuni ya simu na wengine ni TCRA
 
Sasa unafikiri hao TCRA hawakutani na zahma kama hizo?

Hao unamalizana nao kihuni tu

Mi alinipigia juzi kajidai mtoa huduma akiuliza kutaka kujua changamoto za wateja

Nikamuambia changamoto kubwa ni matapeli wanaopiga simu kutumia namba binafsi na wakijidai custumer care wakati nyie mlishatupa muongozo kuwa mtawasiliana nasisi kupitia namba 100

Nikastukia mtu kakata simu

[emoji23][emoji23][emoji23]umenikumbusha wale wapumbavu wapikutana na msukuma pasua kichwa,aliwasumbua wakachoka.

matapeli-acc yako ina shilingi ngapi??

msukuma-milioni 700 laki 9 na elfu 50

msukuma-aaaal nilisahau kweli kuna elfu hamsini.

jamaa wakawa wanashindwa kudraft massage wamtumie maana hataji kiasi kimoja,wakaanza mkwara[emoji1787]

msukuma-fungeni line yangu niwageuze tumbili.
 
Leo nimepigiwa simu na namba 0653608556 akijifanya Mfanyakazi wa Tigo pesa na akasema akaunti yangu ya tigo pesa imefungiwa.

Jamaa akaanza nisomesha na akauliza simu yako ni smartphone au kiswaswadu. Nikasema kiswaswadu, akaniambia nibonyeze namba *37# sikubonyeza na yeye akajua kwamba sikubonyeza na simu yangu ni smartphone. Kilichofuata ni matusi mazito kwangu.

Kero hii imekuwa ni ya kujirudia, binafsi ni mara ya tatu au nne kunipigia na baada ya kuwashtukia wanatukana.

TCRA tusaidieni kuondoa hizi kero. Yaani jamaa anataka kukutapeli na ukishtuka anakutukana. Hii sio sawa. Tusaidieni lasivyo kuna siku tutachukua sheria mkononi kwa watu kama hawa.
Dah! Hawa mbuzi dawa yake ni kuwakatia tu simu kabla hawafikia hiyo hatua yao ya mwisho ya kutukana baada ya kuwashtukia. Yaani ukishagundua tu ni tapeli, kata simu! Au anza wewe kumtykana, halafu kata simu.

Mimi siku zote naamini kati ya tcra, polisi na makampuni ya simu; mmoja kati yao ana mafungamano na hawa matapeli. Maana wasingekuwa wanajiamini kiasi kile.

Mpaka sasa sijaona hata lengo hasa la kusajili line kwa alama za vidole, huku matapeli wakiendelea tu kutamalaki.
 
Back
Top Bottom