KATIKA dunia ya leo ni vizuri kupata ushauri wa wateja au watumiaji huduma au bidhaa fulani endapo unataka kufanya mabadiliko yoyote ya msingi.
ZOEZI la kusajili namba za simu lingelikuwa rahisi sana kama haya yangelifanyika:
1. Fomu za kujazwa ziwe kwenye ofisi za Mwenyekiti wa Mtaa atakayezigawa kwa Balozi wa nyumba kumi kumi,
2. Mteja wa laini yoyote ile atapata fomu yake kutoka kwa Balozi wake,
3. Fomu hii inatakiwa isiwe kwa ajili ya laini moja bali inayomruhusu mtu kuorodhesha laini zote alizonazo kama ni 1,2, 3, 4 au zaidi na maelelkezo mengine muhimu,
4. Mtaja akishajaza fomu hiyo balozi wake atathibitisha kwa namba za vitambulisho au waraka maalum toka kwa balozi kuthibitisha mtu huyo ni mkazi wa eneo lake na maelezo mengine muhimu kama yatakavyokuwa kwenye fomu,
5. Kwa waajiri wenye wafanyakazi wengi nao wanastahili kupelekewa fomu hizo na kuthibitishwa na mwajiri wao papo hapo kazini,
6. Kwa mfano badala ya kumngojea mbunge aende (au wao wanaandikishwa otomatiki) kujiandikisha tigo, zain au zantel au vodacom fomu zipelekwe pale pale bungeni na ofisi za bunge zitathibitisha na wabunge kuwa na simu zilizokwishasajiliwa bunge likiisha baadaye,
7. Kutoka kwa balozi fomu zitarudishwa kwa Mwenyekiti wa mitaa naye atakuwa anazipeleka kwa mtoa huduma na TCRA au wakala wao atakayekuwa anakusanya fomu hizo,
8. TCRA itakuwa inaweka kumbukumbu za usajili wakati wote na kuhakiki ili pasiwe na makosa yatakayojitokeza mwisho wa zoezi,
9. Waajiri watazirudisha fomu hizo moja kwa moja kwa mtoa huduma au TCRA au wakala wake atakayekuwa anafanya kazi hiyo,
10. Upo uwezekano pia wa kutumia mtandao mtu kujisajili ili mradi mtu huyo ana kitambulisho cha kazi, paspoti, akaunti ya benki au cheti cha kupiga kura.
11. Kwa kufanza hivi zoezi zima linaweza kwisha ndan ya miezi miwili tu kutoka sasa na likiwa limekuwa na usumbufu kidogo sana kwa wananchi ambao majukumu yao ya kila siku na usafiri mgumu hasa hapa Dar vinawafanya wawe taabani hata kabla siku haijaisha.
Huu ni ushauri tu na mnaweza kuutupa au kuutumia. KIla la kheri!