TCRA wajifunze kwa Waingereza, kampuni ya simu yalambwa bilioni 33 kwa kuwaongezea gharama wateja

TCRA wajifunze kwa Waingereza, kampuni ya simu yalambwa bilioni 33 kwa kuwaongezea gharama wateja

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Pamoja na agizo la waziri mwenye dhamana ya mawasiliano kuitaka mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano nchini(TCRA) kudhibiti gharama za mawasiliano bado wameonekana kugonga mwamba huku kampuni za simu zikiweka pamba masikioni.

Uingereza sehemu kubwa ya gharama ya mawasiliano ni kwa bili na moja ya kampuni kubwa nchini humo ya O2, wadhamini wa zamani wa Arsenal imekutwa na dhahama ya kulipa faini ya bilioni 33 kwa kuwaongezea wateja wake bili pamoja na kuamriwa kurejesha fedha kwa watumiaji husika.

Ofcom ambae ni TCRA wa Uingereza imesema faini hio ni ukumbusho kwamba watatia mguu endapo wataona kampuni inashindwa kuwalinda wateja wake.
 
Mnataka serikali iingilie kesho mseme inaua biashara? Uzuri ni kwamba kabla ya kununua unajua kabisa Gb1 ni bei fulani hivyo unanunua huku unajua sio kwamba hujui.

Wangapi hapa kwenye biashara zenu serikali inawapangia bei za bidhaa?
 
Hawa wamepigwa faini kwasababu wametoa bill kimakosa kwa miaka zaidi ya 10 kwa wateja fulani. Hawa wetu wamepandisha bei zao na kabla ya kununua unajua ni bei gani. Kupandisha bei sio kosa wewe kama mteja unaweza kuamua kuwakimbia na kuhamia kwenye bei nafuu.
 
Tatizo hamna taasisi ya kumlinda mlaji. Wenzetu hawaathiriki na unyonyaji wa aina hii sababu wana agency ya kumlinda mteja.

Hawawezi kutendewa kinyume na uhalisia sababu wana mtetezi. Ila sisi tuna taasisi zinazoshirikiana na hawa wenye mitandao kuhujumu maslahi yetu.
 
Ukiskia wakubwa wanafaidi basi ndio kama hao TCRA huko,[emoji23][emoji23][emoji23]kila mwezi kuna kibahasha cha wakurugenzi unategemea mtaponaje? Hebu nunueni bando bana acheni kulalamika hovyo bana
Basi angalau wawe wanatupa hizi handsets free,maana pesa kubwa inatumika kwenye vifurushi! Na bila vifurushi handsets zinakua kama kopo tu!
 
Hawa wamepigwa faini kwasababu wametoa bill kimakosa kwa miaka zaidi ya 10 kwa wateja fulani. Hawa wetu wamepandisha bei zao na kabla ya kununua unajua ni bei gani. Kupandisha bei sio kosa wewe kama mteja unaweza kuamua kuwakimbia na kuhamia kwenye bei nafuu.
Kwa hiyo kwa sababu unajua kabisa hakuna pa kukimbilia ndiyo mnatukomoa!? Kisa Makampuni yote ya simu yanashirikiana badala ya kushindana kwenye bei!!
 
TCRA na serikali wanafaidi kitu kwenye huu utapeli.

Kuna gawio nono wanalipata ndio maana huwezi kuwasikia wanafurukuta.

Kwa kweli utapeli wao umekubuhu na unatia kinyaa!

Serikali inapogeuka kuwa chombo cha utapeli ni jambo la aibu.
 
Kwa hiyo kwa sababu unajua kabisa hakuna pa kukimbilia ndiyo mnatukomoa!? Kisa Makampuni yote ya simu yanashirikiana badala ya kushindana kwenye bei!!
Biashara huria.
 
Kwa wakati huu ngumu tunapaswa kugundua njia mbadala za kuendelea japo kuwasiliana na kupashana habari hapa JF.

Issue ya vifurushi na bundle isituache gizani sana kwa akina sisi tusiokuwa na uwezo wa kumudu ghalama.

Kwa ushauri wangu kipindi hiki ile huduma ya FREE BASICS ni muhimu sana kuitumia, ukiwa na Free basics hupati stress za mabei yao ya bundles zao.

Muhimu download apps muhimu kama Facebook lite ambayo ina access moja kwa moja na free basics, app ya chrome itakusaidia pia.

Sasa kwa kupitia Facebook, kama utatumia mtandao wa tigo, utapata search engine muhimu bure kabisa ikiwemo na jamii forums, BBC swahili, Mwananch na nyinginezo nyingi kwa ghalama ya kuwasha data tu.

Ukitumia data ya Airtel, huko utapata search engine nyingi pia, tatizo wao hawana huduma ya JamiiForums.

Pia kwenye facebook lite, ya bure utapata messenger bure na kuendelea kufanya mawasiliano na jamaa zako,

Huduma nyingine kama WhatsApp kwa sasa zione kama anasa nyingine tu.
 
Pamoja na kwamba kuna kadi ya mjasirimali bado huoni hizo gharama zikiongezeka inamrahisihia Magu kukusanya zaidi kutoka kwa wananchi?
 
Hawa wanafanya biashara pamoja. Yaani TCRA ni kama business partner wa makampuni ya simu, lao moja; huyu anapandisha kodi anamwambia mwenzie we wapandishie garama ufidie hapo.
 
Back
Top Bottom