TCRA yaipiga faini ya Tsh. bilioni 11.89 Kampuni ya Intaneti ya Raha Limited kwa kuendesha shughuli zake bila kuwa na kibali

TCRA yaipiga faini ya Tsh. bilioni 11.89 Kampuni ya Intaneti ya Raha Limited kwa kuendesha shughuli zake bila kuwa na kibali

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeipiga Faini ya Sh.bilioni 11.89 Kampuni ya Raha Limited watoa huduma ya Internet kwa makosa mbalimbali ikiwemo kutumia masafa ya mawasiliano ya Radio katika wigo 1452-1482 MHZ bila kuwa na leseni halali kutoka TCRA tangu 24 Machi 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi James Kilaba amesema TCRA ilitoa leseni ya matumizi ya huduma za mawasiliano kimkoa, Leseni ya miundombinu ya mawasiliano, Leseni ya Kitaifa ya matumizi ya mawasiliano ya kieletroniki, leseni ya kufunga na kutengeneza vifaa vya Mawasiliano na Leseni ya matumizi ya namba kwa muda tofauti tofauti.

Mhandisi Kilaba amesema kampuni ya Raha baada ya kupata leseni walitakiwa kufanya mambo mbalimbali ikiwa kujenga,kusimika, kutunza ,kutumia na kusimamia miundombinu ya mikoa ya Dar es Salaam,Arusha na Tanga ifikapo Februari 2020 na Kilimanjaro ifikapo Septemba 2021 pamoja na kuandaa na kuwasiliasha mpango wa kuendeleza rasilimali Watu kwa Mamlaka hiyo.

Amesema kuwa katika kufanya kazi waliweza kuchukua masafa ya mawasiliano ya Radio mkoani Mtwara bila kubali na kupigwa faini sh.Bilioni 11.85.

Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Kilaba amesema kampuni Raha wanatakiwa kulipa faini sh.milioni 10 kwa kujenga Miundombinu ya mfumo wa mawasiliano kuendesha na kutoa huduma za mawasiliano mkoani Mtwara bila ya kuwa na Leseni kutoka TCRA, Kulipaa Faini ya Tsh. milioni 5 kwa kutotimiza masharti ya Leseni baada ya kushindwa kutoa huduma mkoani Kagera Agasti 2019.

Aidha amesema kampuni hiyo inatakiwa kulipa Tsh.milioni 5 kushindwa kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa mahesabu ya ndani ya miezi sita kuanzia mwaka wa hesabu na sh.milioni tano zingine ni kushindwa kuwasilisha mpango mkakati wa kuendeleza rasilimali Watu huku faini nyingi Tsh. milioni 10 kushindwa kutimiza masharti ya leseni hususani kushindwa kuomba upya kwa muda uliopangwa.

"Masafa ni rasilimali ya Taifa haikopwi wala haiibwi na mtu yeyote."Amesema Kilaba.

Chanzo: Isaamichuzi blog
 
Kama kila kitu tunaona upuuzi acheni Tz liwe shamba la bibi majengo ya hizi tasisi tupigie rumba.

Mwenye uwezo wa Redio, Tv Kuvua samaki , ikiwa ni Uwindaji au chochote tusimbugudhi, maana ni uupuzi kila serkali ikfanya.

Lkn hakika ukienda kwao hata ku puuu utalipia kodi.

Yaani rushwe matangazo ya redio bila kulipia, thubutuuuu. Yaani sijui kwanini tujidharau hivi? Tuko inferior kwa hawa jamaa mpaka wanatushangaa.
 
Back
Top Bottom