TCRA yapiga marufuku wimbo wa Nay wa Mitego uitwao "Tozo"

TCRA yapiga marufuku wimbo wa Nay wa Mitego uitwao "Tozo"

Unbef*****livable..., Really WTF....., Huyu mama anageuka JPM kila siku bila mazuri ya JPM, Yaani hii ni worse case Scenario.....

By the way nilikuwa sijausikia na huenda nisingeusikia sasa ngoja nikausikilize....
 
Ney hajawahi ni disappoint nahis anastahili tunzo maana amejitoa kuwawatetea wananchi walalahoi kupitia sanaa, watu Kama hawa siku wakuondoka duniani ndio utasikia Sifa za wanafiki.

Wangapi wanaweza kufanya hichi anachofanya Ney kwenye nchi inayoongozwa Na viongozi wa kiwaki wa ccm ambao ukijaribu kumkosoa anatishia kukutoa uhai? Kiufupi Jamaa amejitoa muhanga mpeni Sifa zake msisubir mpaka afe ndio muanze kumsifia, wengi wetu humu ni keyboard warriors waoga kama mbwa koko.
 
jimmy-elmo-1.gif

Freedom of speech!! Bonge la Ngoma!!
 
Ilimradi kila mwenye akili timamu anao kwenye simu yake wao wafungie tu. Na kwenye magroup ya Whatsapp tutatumiana kila Mtu awe nao.
 
View attachment 2366404
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imetoa agizo hilo kwa vyombo vyote vya Utangazaji nchini baada ya kupokea taarifa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa BASATA.

Kwa mujibu wa barua ya TCRA imesema baada ya BASATA kuhakiki wimbo huo imebaini kuwa maudhui yake hayafai kutumika katika jamii na yanaweza kuleta matokeo hasi.
View attachment 2366584
Kwani huo wimbo unashida gani kama msanii amewakilisha ujumbe wake tena amechuja sana tofauti na wananchi wanavyowasema vibaya watalawa?

Uonevu wa kiwango cha juu, serikali iliyoko madarakani immpaka matope na uchafu wote hayati JPM kujipatia sifa za kisiasa ambazo hata hivyo zimeshindikana kupatikana sasa wanajidhihirisha kwamba wao ndio waliokuwa wamamchafua kwa ubinafis wao
 
Ukisikia promotion ndio hii...nilikuwa sijui hata kama kuna wimbo kama huu ila TCRA mmenifaa sana..ngoja niutafute
 
Kwani sisi wabongo ni washamba kiasi hicho? Huu wimbo hauitwi Tozo, and was uploaded a year ago. Nimetafuta wimbo wa "Tozo" YouTube, ila sijaupata.
 
Ndo wameupa umaarufu huo wimbo.. binafsi nilikua siujui kabisa ila sasa inabidi niutafute niusikilize
 
Nchi imefunguka! Watu wako huru kufanya wapendacho.
 
Hawaelewi waguse wapi maskini ya Mungu serikali kila sehem kwa moto
 
Kwahiyo maudhui ya ule wimbo wa "CCM ni ile ile tutaisoma namba" ndio yanafaa kusikilizwa na umma wa Watanzani?

Kama Propaganda zizuiwe zizuiwe pande zote, sio upande wetu Wapinzani tu,hawa BASATA wasitumike kama Jumuiya za CCM.
 
Back
Top Bottom