Kamati ya Maadili ya TCRA imesema Kituo cha Star Tv kimeonesha uzembe na udhaifu katika kusimamia kipindi cha EFATHA Ministries ambacho hurushwa kwa matangazo ya moja kwa moja, kwa kuruhusu maudhui yenye ukakasi ambayo ni kinyume na Kanuni za Mawasiliano
TCRA ikimnukuu Askofu Josephat Mwingira imesema maneno yake kwamba "Serikali fanyeni upuuzi wenu Mungu amewaruhusu, lakini muda sio mrefu atakuja kumalizana na upumbavu wenu" yanafedhesha kutokana na Lugha isiyo na staha kwa Mamlaka ya juu ya Nchi
Kipindi cha EFATHA kimesimamishwa kwa miezi mitatu, huku Star Tv ikipewa onyo na kuamriwa kuomba radhi watazamaji na umma kwa siku tatu mfululizo kuanzia Januari 25 - 27, 2022
Kwa hiyo lile tamko la Simbachawene na Muliro la kumtaka huyo Askofu na Nabii Mwingira kuripoti kituo cha polisi kati ndani ya masaa 24, ndiyo limeishia hapa sasa!
Bila shaka Askofu ameshinda. Maana ujumbe umefika. Serikali iachane na mambo ya kipuuzi na kipumbavu! Badala yake itumie nguvu kubwa kuwaletea wananchi maendeleo.
Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) imesema Kituo cha Star Tv kimeonesha uzembe na udhaifu katika kusimamia kipindi cha EFATHA Ministries ambacho hurushwa kwa matangazo ya moja kwa moja...
Sidhani kama TCRA watamfunga mdomo kwa style hiyo, huyu mtu naona muda wake wa kuongea umefika, ni kama vile alikuwa anateseka kwa kujiuliza nafsini mwake aseme au anyamaze, sasa ameamua kusema kwake liwalo na liwe, heri awe na amani ya nafsi kuliko kumfurahisha mtawala huku akikosa amani ya nafsi yake.