TCRA: Yatoa neno kwa Vyombo vya Habari vinavyowatumia watangazaji wasio na Taaluma ya Habari

😁😁😁
Kwani Kina Lokole na Baba Levo ndio Walioomba hiyo kazi ama UTAWALA uliamua?!!!

Isije ikawa vetting ya kupata faida zaidi imefanyika zaidi kuwa recruit halafu wewe unakalia HISIA..πŸ˜‚πŸ˜‚
Sasa wasafi wasubiri kufutiwa leseni.
 
Nawaza Hapa.....

Hivi mtu anataka kuwe na MWANATAALUMA wa habari,kwenye kipindi Kama MASHAMSHAM Cha WASAFI FM?!!!

Huyo mwanataaluma atadeliver vyema ubora kwa wateja wao kama hao kina Dida,Babu Iddy na Ankali Mambi?!!!

Nikiwa Kama Msomi nilikuwa Sina mzuka kabisa wa kusikiliza vipindi Aina hiyo,ila ninavyozidi kukua kifikra huwa nikiwa OFF DUTY huwa ninawasikiliza vyema tu ili kuwafahamu maisha ya wenzetu wa uswazi lakini pia kutoa STRESS ZA MIHANGAIKOπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Basi walau wawe update na sheria na wajue nini inatakiwa iende hewani na ipi haitakiwi.
 
Aache fujo alete makaratasi
Ha ha ha Kwako Makaratasi Yana Umuhimu Sana kuliko INTELLECT eee?!!!
Mbona Kuna WASOMI kibao wanapata Makaratasi kwa mbeleko za kubebwa,kupendelewa,mahusiano TATA...halafu kichwani ni taburarasa Tofauti na GPA zenye mng'aro...πŸ˜‚πŸ˜‚

Haya Mkuu Wangu.
 
Huyu jamaa Ni jembe!
 
Ilitolewa Miaka mitano kuanzia 2016 mpaka 2021 sasa Kama mtu anataka kuwa mtangazaji na hajasomea awaachie waliosomea.
Hata uijue Sheria vipi huwezi kusimama mahakamani Kama advocate mpaka uidhinishwe kuwa advocate.
Lakini naona taaluma zingine Kama uandishi wa habari kila mtu mradi anajua kuongea anakuamwandishi wa Habari.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Hivi kunatofauti kati ya "journalist" na "Presenter"..?
 
Ni jambo zuri kama serikali imefikia mahari na kuona umuhimu na kudhamini swala la profesionalism katika kazi basi ni sawa ,

Lakini na jaribu tu kufikiria kama kweli serikali ina maanisha hicho inachokisema ,mbona bado tunaendelea kuona madudud yale yale yakiwa yanataka kutokea upande mwingine ? .

Ukweli lazima usemweme , kama serikali imeona kufanya kazi ya utangazaji pasipo kuwa na taaluma ya utangazaji ni kosa kisheria , je kuajili wa watu ambao hawana taaluma ya ualimu wakawe waalimu tena bira ya wafunzo yoyote yatakayo wafanya waendane na fani ya ualimu , kisheri hii imekaaje ?..

Ushauri wangu kama tumeamua kuheshimu swala professionalism basi hili swala lisiishie huko tu kwenye utangazaji sheria hii ipite kote kwenye taasisi zote binafsi na taasisi za umma , na kama hilo haliwezekani basi tuache tu mambo yaende kama yalivyokuwa yanaenda lakini siyo huku kigezo hichi kinazingatiwa lakini kule kigezo hicho hicho hakizingatiwe huku ni kuharibiana kazi .
 
Yule Dr Isaack Mzee wa Njia Panda vipi? KASOMEA UANDUSHI AU UDOKTA?
 
Safi sana aisee nimekuwa nikiongea hili mara nyingi mno, watu hawataki kusoma mwishowe wanavamia kazi za watu, hili tatizo limekuwa kubwa nchini, tunaambiwa ajira hazipo lkn kiuhalisia zipo lkn wanaajiriwa watu wasio na ujuzi, ifike wakati tuache kuchekeana unakuta mtu kasoma ualimu lkn yupo benki kisa kuna ndugu yake benki husika.

Kuna kazi nyingi wanakaa watu wasio na sifa, mfano hata ubunge eti kigezo ni kujua kusoma na kuandika what a joke!!! Wakati tungeweza kuambiana ukweli kwamba inampasa mbunge awe na atleast degree, diwani atleast diploma vivyo hivyo wenyeviti wa serikali za mitaa.

Tunalalamika ajira hakuna wakati zipo, tunaharibu thamani ya elimu kwa kuendekeza siasa mwishowe hao hao wasio na elimu wanaanza kutukana elimu yetu je unadhani watoto watakuwa na hamu ya kusoma?

Tuache siasa tuweke uhalisia kwa kuzingatia professionalism, ifike kipindi kila idara kuwe na watu wenye taaluma ya kazi husika, ubabaishaji hautatufikisha popote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…