Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), chini ya mamlaka iliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Sura ya 306, na Kanuni zake ina wajibu wa kusimamia huduma za mawasiliano ya Simu na Intaneti, Posta, na Utangazaji wa Redio, Televisheni na Maudhui Mtandaoni.
Hivi karibuni kumekuwa na watoa huduma za Maudhui Mtandaoni wanaosambaza Habari na Matukio wasio na leseni kinyume cha Sheria na Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2020 na marekebisho yake ya mwaka 2022.
TCRA imekuwa ikifuatilia kwa karibu mwenendo wa utoaji huduma za maudhui mtandaoni na inachukua nafasi hii kutoa onyo kali kwa wale wanaokiuka sheria na kanuni za huduma za utangazaji. TCRA haitasita kuchukua hatua kali kwa wale wote wanaojihusisha na kutoa huduma hizi bila leseni kwa kuwafikisha katika vyombo vya Sheria.
Vilevile, TCRA inapenda kuwakumbusha Watoa Huduma za Mawasiliano ya Simu (Mobile Network Operators - MNOs) na 'SMS Aggregators' kuhakikisha kuwa:-
1. Maudhui ya arafa za mkupuo (bulk messages) kuelekea, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu 2025 yanazingatia Sheria na Kanuni zote za mawasiliano ya Kielektroniki na Posta.
2. Uhakiki wa maudhui (content vetting) unafanywa kabla ya kusambaza arafa za mkupuo zinazohusika, ili kuhakikisha hakuna ujumbe wenye kuchochea vurugu, uvunjifu wa amani, au kueneza taarifa za uongo (misinformation) unaowafikia watumiaji wa huduma za mawasiliano.
3. Maudhui yote yanayohusiana na shughuli za Uchaguzi Mkuu yanapata idhini kutoka kwa taasisi au uongozi wa chama cha siasa husika.
4. Watoa huduma wanapaswa kuhifadhi kumbukumbu za arafa zote zinazotumwa kwa wingi kwa kipindi kinachotakiwa kisheria kwa ajili ya uthibitisho endapo utahitajika.
TCRA inatoa wito kwa wadau wote kushirikiana katika kuhakikisha mawasiliano na maudhui yanayotolewa kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 yanadumisha amani, mshikamano wa kitaifa na uhalisia wa taarifa kwa wananchi.
Imetolewa tarehe 16 Agosti 2025.