TCRA yawafungia Wasafi FM kwa kutumia lugha za matusi

TCRA yawafungia Wasafi FM kwa kutumia lugha za matusi

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha utoaji huduma za utangazaji kwa Wasafi FM kwa muda wa siku saba kuanzia Septemba 12 hadi Septemba 18 mwaka huu.

Uamuzi huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba Jijini Dar es Salaam ambapo amesema hatua hiyo ni kutokana na kituo hicho kukiuka kanuni namba 11 ya Kanuni za Mawasiliano ya kielektroniki na Posta ya mwaka 2018.

Mhandisi Kilaba amesema kuwa ukiukwaji huo wa kanuni ulifanyika katika vipindi vya The Switch na Mashamsham.

Aidha, ametoa rai kwa vyombo vya habari kuzingatia kanuni za utangazaji wa maudhui yenye lugha ya staha kwa Watanzania huku akiitaka Wasafi FM kuomba radhi kwa umma wa Watanzania.

Tcra.jpg

Maendeleo hayana vyama!
 
TCRA imekifungia kituo cha utangazaji cha Wasafi Fm baada ya watangazaji wake na mgeni wao baba Levo kutumia lugha za matusi na zinazoudhi mbele ya jamii.

Mfano neno " msambwanda" linakarahisha

Kituo cha Wasafi hakikuwa hewani kwa muda wa siku 7 kwa mujibu wa adhabu waliyopewa.

Maendeleo hayana vyama!
Kwakweli WAfungiwe tu, hakuna namna, HAPA KAZI TU.
 
Ila niliitazama kile kipindi kiukweli TCRA wanakahaki ya kufungia stesheni. Yaani kipindi kimekosa maudhui hadi basi.....

Baba levo aliulizwa swali kuwa kati ya mwanamke mnene mwenye shepu na wembamba ni yupi anapendelea....

Baba levo akajibu yeye wanawake wanene/mabonge asichowapendea ni wanachoka haraka kitandani halafu wanakuharakisha na wewe ukojoe haraka haraka, so yeye huwa anachofanya anawakojolea mkojo wa kawaida na sio bao lile bao la utamu.....




Katika hali ya kawaida mazungumzo ya namna hii hayana hadhi ya kurushwa hewani as if ni jambo la kawaida na wakati ni kinyume na maadili yetu ya kitanzania na kiafrika lakini mbaya zaidi inachochea maswala ya ngono.
 
Back
Top Bottom