TCRA yazifungia Laini 21,000 zilizohusika kufanya utapeli

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
ZAIDI ya laini 21,788 za mawasiliano ya simu zimefungiwa kupokea na kutoa mawasiliano kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kutumika kufanya uhalifu mtandaoni kwa kipindi cha miezi mitatu iliopita.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwenendo wa sekta ya mawasiliano iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari, idadi ya matukio ya ulaghai imeendelea kupungua kutoka laini za simu 23,328 zilizofungiwa Julai na Septemba 2023 hadi laini za simu 21,788 kwa Oktoba hadi Desemba 2023 ikiwa ni upungufu wa laini za simu 1,540, sawa na asilimia 6.6.

Aliitaja mikoa inayoongoza kwa matukio ya simu za ulaghai hadi kufikia Desemba mwaka 2023 na idadi ya kwenye mabano ni Rukwa (7,666) na Morogoro (7,171), Dar es Salaam (1,717), Mbeya 1,549, Tabora 590 na Songwe 328. Mikoa yenye matukio machache ni Kaskazini Pemba (5), Kusini Pemba (6) na Mtwara (22).

Dkt. Bakari alisema TCRA imeendelea kubaini simu za ulaghai zinazoingia nchini na hatua stahiki zimekuwa zinachukuliwa ambapo idadi ya simu za udanganyifu imeendelea kupunguwa.

Chanzo: Nipashe
 
Jamaa huwa wanajua kulenga...
 
Kilimanjaro hawamo Kwa wizi wa simu Kwa mamlaka ninayojipa mwenyewe bila kupewa kibali na Papa Natangaza rasmi kuwa wachaga sio wezi ni watakatifu papa awatangaze kama watakatifu wachaga wote kuanzia leo
 
Wamiliki wa hizo laini wakitaka kusajili laini zingine wanatakiwa wajisalimishe kwanza TCRA kujibu tuhuma
 



Kupokea ujumbe wao ukiwa unasona uzi huu ni dhahiri kuwa tuna uhalisia tofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…