Ndg wanajamii, Kuna tetesi kuwa eti Serikali walisitisha kutoa matokeo ya mchakato wa usajili ili kuwajumuisha watoto wa 'Vigogo' waliokuwa wakisoma 'Cambridge'. Binafsi inanisikitisha sana;
1. Kwa nini hili halikufanyika mapema ili taratibu za uombaji ziweke wazi kuwa matokeo yatatoka kipindi fulani? Ni imani yangu kuwa suala la kuchelewa kuhitimu kwa hao wanafunzi wa Cambridge kulijulikana mapema kwa yeyote ambaye angehitaji.
2. Katika 'website' ya TCU kuna ujumbe unaoonyesha kuwa matokeo 'yatatangazwa' katika mwezi Julai! Sijui hiyo Julai inayosemwa ni ya mwaka 2012!, au ipo kwa bahati mbaya! Ni muhimu watanzania tukajifunza sasa kuwajibika kwa wakati!
3. Lipo tangazo la TCU linalotoa nafasi kwa waombaji ambao hawakuomba awali (naamin hawa ndiyo Cambridge, walengwa hasa wa tangazo na ucheleweshaji wa matokeo!) na wale walioomba awali wakakosa nafasi! Swali langu hapa ni Je, mtu atajuaje kuwa hakuchaguliwa, ili hali matokeo yenyewe hayajui? Imani yangu hapa ni kuwa huu ni mwendelezo wa 'USANII' wa serikali yetu(?). Na Je, 'usanii' huu ni kwa manufaa ya nani?
4. Matokeo hayapo (hiki ni kipindi ambacho yalipaswa kuwepo, rejea Na. 2 hapo juu) wala hakuna tangazo jipya linalosema ni lini yatatoka! Je, usiri huu nao ni kwa manufaa ya nani?
WITO
1. Ikiwa ni busara, naomba tujadili suala hili kabla wanafunzi hawajagoma au CHADEMA kuandamana.
2. Watumishi tuwajibike, japo hatujazoea!
Mimi ni mtumishi wa serikali, nadhani ni busara kutambua kuwa watumishi tupo kwa ajili ya wananchi ambao ndiyo waajiri wetu! Tusipobadlika kuanzia sasa, tutabadilishwa na 'mafuriko' na gharama yake itakuwa kubwa na wala hatutaimudu kamwe!
Nawatakia kila la kheri wale wote wanaosubiri matokeo kwa uchu, lakini zaidi nawapa pole wale watakaokosa nafasi kutokana na nafasi zao kuchukuliwa na 'Wanacambridge'