DOKEZO TCU ifanye ukaguzi wa mara kwa mara vyuoni kuzuia wanafunzi kuwekewa mafungu kwenye Ada ambayo hayatekelezwi

DOKEZO TCU ifanye ukaguzi wa mara kwa mara vyuoni kuzuia wanafunzi kuwekewa mafungu kwenye Ada ambayo hayatekelezwi

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimanjaro Christian Medical University College(KCMUCo), naiomba tume ya vyuo vikuu Tanzania(TCU) iwe inafanya ukaguzi kwenye vyuo kujiridhisha kama utaratibu uliowekwa na chuo husika una uhalisia na unatekelezwa

Mfano katika chuo tunatakiwa tulipe bima ya afya mara mbili ambapo hela ya bima tunailipa pamoja na ada ya shule, na muda huo tunatakiwa tutengeneze control number ya kulipia BIMA pekee na kufanya hela ya bima kulipa 100,800 badala ya 50,400

Kingine kuwekewa mafungu ya community field na ilihali kuanzia mwaka WA TATU(MD3) hakuna ratiba ya community field
 
Chuo kunakuaga na Medical Fees, ni tofauti na Bima.
 
Tunaishauri tume ya vyuo vikuu Tanzania(TCU)kufanya ufatiliaji kwenye vyuo vikuu kuona ada inayolipwa kama ni halisi.

Katika chuo changu cha KCMC, wanafunzi tunalazimika kulipia bima mara mbili na hela nyingine kama za community outreach ambazo kikawaida hufanyika kwa miaka miwili tu, lakini tunalazimika kulipa kwa miaka yote mitano. Hii inaongeza mzigo wa ada kwa wanafunzi
 
Back
Top Bottom