Duu kwahiyo nyumbu 600 ni sawa na Simba mmoja? Wakati mwingine sifa za kuwa VC hazifahamiki zaidi ya kuwa Senior kitaaluma, yaani yule mwenye publications nyingi, professor wa muda mrefu na WA dini, kabila, Chama gani Cha siasa na rafiri wa anaemteua vinahusika sana.
Haizulu basi angeambiwa angalau awe na hata kidiploma Cha uongozi au ikishindikana apelekwe ngurudoto akapate semina elekezi juu ya kuhudumia wenzake. Kosa la wanasiasa ni kudhani kuwa ukiwa professor basi unafahamu kila kitu hapa duniani, yaani professor hahitaji tena kuwa na teaching methodology, leadership and management skills au chochote maana anajua kila kitu, na hapo ndio tunapofeli, na elimu yetu inaishia hapohapo.
VC anaishia kukinga mikono apewe hela za tafiti, mishahara, kulipa umeme, maji na hata kujenga choo. Vyuo vikuu vinageuka ombaomba kwa vyuo vya Ulaya, wanaagiza hata vitabu vya kufundishia wanafunzi wao, hakuna Mwl anaeandika vitabu. Wanafanya tafiti za kughushi TU kwa kudandia zile za wanafunzi ili wapate promotion, tafiti zinazofungiwa makabatini badala ya kugeuka projects za kutatua shida za jamii walizoziona.