Team Buying(Group Buying)

Team Buying(Group Buying)

Investaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2015
Posts
819
Reaction score
756
Habari wazee wa business.

Kwenye kuzurura mtandaoni nimekutana na business idea ambayo inaweza kutumia ata hapa bongo na kufanya vizuri, nimegundua hili baada ya kwenda kkoo kununua vitenge vya jumla nakuona ambavyo sipat faida kubwa kama ningenunua kama team/group. Kuna winga uwaga namtumia kwenye vitenge kkoo ndio akanisanua kuhusu mchezo wanaoufanya wafanyabiashara wa kariakoo na kupata faida kubwa kwa mtaji mdogo.

Ukienda kwa mhindi mnazi mmoja wananuna vitenge ad 8k kwa doti 1(3pics) kwa ua moja nadhan wauza vitenge mnanisoma kwa uzuri ninavyosema ua moja. Na kila mfanyabiashara anaunua doti 40 yaan vitenge 40 vinavyofanana maua. Unakuta wapo wafanyabiashara 10, kwahiyo kila moja ananuna doti 40 kama mwenzake ila ua tofuati; ukijakumjulisha wamenunua vitenge 400(doti 400), baada ya kununua wanabadilishana maua kila mtu anapata ua moja moja kila doti kwenye doti 40. Kumbuka mtaji wake ni 8k x 40 = 320k. Ukiwa pekeyako uwezi pata doti 40 kwa maua tofauti kwa sh 8k. Ukienda kwa mhindi kununua doti 40 utapata kwa sh 8k ila maua manne; maana mhindi anauza ua moja kwa doti 10. Uknunua doti 40 ukiwa pekeyako unakuwa na maua manne kitu ambacho kitakugharimu kwenye kuuza , utapiga navyosana picha ad umalize ila ukiwa na maua tofauti ni rahisi sana kuuza fasta kama wanavyofanya wafanyabiashara wa kkoo.

Faida ni kubwa sana, mtaji 320k vitenge 40; kkoo vitenge wanauza 13k/15k ukikaa vibaya, madharan unauza 12k kwenye vitenge 40 anatapa 480k. Faida ni 120k. Huu ndi mchezo unachezeka kkoo ambao unasaidia kukuza mtaji fasta.
Huu mchezo wa kununua bidhaa kama Team ulianza CHINA, ukiingia google utaona kwenye wikipedia utapata maelezo haya:

"
Group buying, also known as collective buying, offers products and services at significantly reduced prices on the condition that a minimum number of buyers would make the purchase. Origins of group buying can be traced to China, where it is known as Tuán Gòu (Chinese: 团购), or team buying.[1]

In recent times, group buying websites such as Pinduoduo in China have emerged in the online shopping business. Typically, these websites feature a "deal of the day", with the deal kicking in when a set number of people agree to buy the product or service. Buyers then print off a voucher to claim their discount at the retailer. Many of the group-buying sites work by negotiating deals with local merchants and promising to deliver a higher foot count in exchange for better prices.

"

Baada ya kuelewa huu mchezo natafuta wafanyabiashara wadogo wadogo ambao tunanuna bidhaa ambazo zinafanana kwende kkoo na sisi tupate faida kubwa kama wenzetu wa kkoo. Nilizurura sana j3 kutafuta machimbo ya shuka za KAMPALA kule mnazi mmoja, nikuta duka moja la mhindi wanauza 35k ambapo unapata shuka 2 foronya 4, tukienda watu 10/20 kunauwezakao mkubwa sana wa kupunguziwa bei hadi 30k/29k.

Pia na vitenge kama mpo tunaweza tukakusanyana tukaenda kwa mhindi tukachukue vitenge ata kila mmoja akichukua doti 10 sio mbaya. Mtaji ni 80k kila mmoja ingawa mm uwaga nachukua 100, ila tutaenda kwa kuongeza idadi kutokana na mzunguko. Kuna vitu vingi ambavyo tutakuwa tuna organize kununua ambavyo ni vya kwenda pale kkoo. Vyombo navyo ni mori set ni 36 ukinunua vingi at 30 unanunua.

Kwa mtu ambaye yuko dar na amependa hii business idea tunaweza tukawa na group la whatsapp tukajadili vyema hili swala maana ni mchongo pesa ambao unaweza kukusaidia kukuza mtaji wako kwa haraka zaidi.


Last words, unaweza ingia google ukasoma zaidi kuhusu TEAM BUYING/GROUP BUYING ; hakuna risk kama wote tunaenda kununua bidhaa duka moja na kila mtu anachagua ua kama tutadili na vitenge au tunaweza kujadiliana maua tukiwa kwa mhindi ili tupate bidhaa bora ambayo itakuwa ni mori kwenye market.

Watu wanaouza boxa na vest kama mtapatikana tujikusanye twende tukachote mzigo kwa bei chee tukiwe wengi, maana mchikichini boxa box 4 ni 29k; tukinunua mzigo mkubwa bei inashuka zaidi.

Mnaweza nichek whatsapp 0652247221. Mengine tutadiskas kwenye group .
 
Samahani mkuu nje ya madakama hutojali naomba msaada wa kujua wapi nitapata kwa Bei ya jumla mazulia ya kufutia miguu
IMG-20221128-WA0017.jpg
 
Ukishanunua hivyo vitenge unauza chap au unakaa kama machinga kusubiria mteja mmoja mmoja.
 
Samahani mkuu nje ya madakama hutojali naomba msaada wa kujua wapi nitapata kwa Bei ya jumla mazulia ya kufutia miguu View attachment 2430572
Nenda pale china plaza kuna road nyooka nayo upande wa kushoto utaona frem zimejificha hatare ingia hapo kuna mazaga kama yote bei chee.
 
Lengo sio kuuza kwa jumla bali kuanza biashara kwa mtaji mdogo lakini faida kubwa ili ukunze mtaji wako fasta na kuendesha maisha yako vzuri, madharani unataka kuuza jeans, ukienda kwenye duka la jumla jeans unaweza nunua kwa sh 9k/10k; kuna siku nilikuwa na jamaa angu kkoo alitoka mkoa tulijuana kupitia telegram, so akaja dar kunichek tukaenda kkoo kununua jeans. Tulizurura sana kkoo tukaingia machimbo ya ndan kabsa tukakuta jeans zinauzwa 14k nilijiunza mara 2 izi sio zile ukipanda boda zinachanika. Jamaa angu akachukua moja mm nikasita sikuchukua maana nimezoea kununua jeans 18k.

Jamaa anarud mkoa nikamuliza ile jeans niaje, iko fresh haina shida yoyote ...

Kama wanauza 14k rejareja kuna sehemu wanachukua chini ya hapo, swali la kujiulza ni wapi; sio lazima kununua jeans za kuuza unaweza nunua ata za kuvaa wewe. Ni rahisi kununua jeans 10 kwa 90k kuliko kununua jeans 10 kwa 180k. Tukiwa group bidhaa nyingi tunanunua kwa bei ya chini 🙂. Hii trick inabid tuitumie kwa sana ilitupunguze gharama ya maisha. Badala ya kununua boxer moja 5k , unanunua boxa box 4(boxa 12) kwa 29k.


Haya yote yanawezekana kama tukiwa group buying/team buying. Tukitaka jeans, vest, boxer , raba n.k.
Kama upo interested kwenye group la kununua bidhaa(TEAM BUYING/GROUP BUYING). Unaweza nichek niunde group tuanze ku enjoy maisha, pia tunaweza jadili mambo mengine ya biashara kwa kununua bidhaa au huduma kwa group.

Ukijikita kwenye utafiti wa team buying kwenye google utagundua yapo ya aina nying sana magroup ya design hii mengine ni REAL ESTATES: hapa tunaweza nunua apartment then tukapangisha. Endelea kula mchimbo utagundua TEAM BUYING inafaida kubwa sana kama mtajua namna ya kupiga pesa sokoni.
 
Wajamani ukija njoo whatsapp sinaga message za kawaida. Group lipo tayari njooni sasa tujadili tunaanza na bidhaa gani za kuvaa au kuuza. Karibu sana wazee wa business , huu mchongo fanya usikupite. Ata wa mkoan njoo mm nitasimamia pesa zako sinaga mbambamba kwenye pesa.
 
Back
Top Bottom